Pata taarifa kuu
MYANMAR

Jakarta yataka kusitishw kwa machafuko na kurudi kwa demokrasia Myanmar

Rais wa Indonesia Joko Widodo ametoa wito kwa viongozi wa kijeshi nchini Myanmar na pande pinzani kusitisha machafuko na kurudi kwa demokrasia nchini humo baada ya mkutano wa Wakuu wa mataifa ya Jumuiya ya nchi za kusini mashariki mwa Asia, ASEAN, kuhusu mgogoro nchini Myanmar.

Wakuu wa mataifa ya Jumuiya ya nchi za kusini mashariki mwa Asia ASEAN wamekutana na jenerali mwandamizi na kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Myanmar katika mkutano wa dharura wa kilele uliofanyika Indonesia Jumamosi Aprili 24, 2021.
Wakuu wa mataifa ya Jumuiya ya nchi za kusini mashariki mwa Asia ASEAN wamekutana na jenerali mwandamizi na kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Myanmar katika mkutano wa dharura wa kilele uliofanyika Indonesia Jumamosi Aprili 24, 2021. via REUTERS - Indonesian Presidential Palace
Matangazo ya kibiashara

"Hatua ya kwanza jeshi la Myanmar kusitisha matumizi ya vurugu na kwamba pande zote zijizuie ili kupunguza mvutano," amesema kiongozi wa nchi hiyo kubwa katika ukanda huo. "Vurugu zinapaswa kusitishwa, utulivu na amani nchini Myanmar lazima virejeshwa."

Wakuu wa mataifa ya Jumuiya ya nchi za kusini mashariki mwa Asia ASEAN wamekutana na jenerali mwandamizi na kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Myanmar Min Aung Hlaing katika mkutano wa dharura wa kilele uliofanyika Indonesia leo Jumamosi.

Kiongozi wa taifa hilo Aung San Suu Kyi na viongozi wengine wa kisiasa bado wanashikiliwa pasipojulikana.

Kumeshuhudiwa maandamano yaliyogubikwa na machafuko ya kupinga mapinduzi hayo na kusababisha vifo vya mamia ya waandamanaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.