Pata taarifa kuu
ARMENIA

Mauaji ya kimbari ya Armenia: Uturuki yamwitisha balozi wa Marekani

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amemuitisha balozi wa Marekani nchini Uturuki Jumamosi wiki hii ili kupinga hatua ya Rais wa Marekani Joe Biden ya kutambua mauaji ya halaiki ya Armenia, shirika la habari la serikali Anadolu limeripoti.

Rais wa Marekani, Joe Biden ametambua mauaji ya Waarmenia ya mwaka 1915 yaliyofanywa na askari wa utawala wa Ottoman kama mauaji ya kimbari.
Rais wa Marekani, Joe Biden ametambua mauaji ya Waarmenia ya mwaka 1915 yaliyofanywa na askari wa utawala wa Ottoman kama mauaji ya kimbari. Getty Images via AFP - MARIO TAMA
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Uturuki hapo awali ilikuwa imetangaza: "Tunakataa na kulaani kwa maneno mazito tamko la rais wa Marekani kuhusu tukio la mwaka 1915".

Rais wa Marekani, Joe Biden ametambua mauaji ya Waarmenia ya mwaka 1915 yaliyofanywa na askari wa utawala wa Ottoman kama mauaji ya kimbari.

Biden ni rais wa kwanza wa Marekani kutumia neno mauaji ya kimbari katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mauwaji hayo, siku moja baada ya kumjulisha Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan juu ya uamuzi huo.

Uruguay, Ufaransa, Ujerumani, Canada na Urusi zilitambua mauaji hayo ya kimbari, lakini Marekani haikuwahi kutangaza rasmi chini ya marais wengine hadi rais wa sasa Joe Biden.

Uturuki inapinga kuwa mauaji hayo ya Waarmenia ni ya kimbari. Rais Erdogan amesema mijadala kuhusu mauaji hayo inapaswa kufanywa na wanahistoria na sio wanasiasa, amesisitiza kuwa maneno hayawezi kamwe kubadili historia.

Armenia kupitia Waziri wake Mkuu, Nikol Pashinyan, amemshukuru rais wa Marekani Joe Biden kwa hatua hiyo muhimu ya kulinda haki. Alisema imepokelewa kuwa ni ushindi mkubwa kwa Armenia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.