Pata taarifa kuu
INDONESIA

Indonesia: Hakuna matumaini ya kuipata manowari iliyopotea

Marekani imepeleka ndege ya P-8 Poseidon kushiriki katika shughuli ya utaftaji na uokoaji wa manowari ya Jeshi la Wananchi la Indonesia iliyopotea katika Bahari ya Bali, huku kukiwa na matumaini madogo ya kupata wafanyakazi 53 wa manowari hiyo wakiwa hai.

KRI Singa-651, meli ya kikosi cha majini cha Indonesia ikiondoka bandari ya Tanjung Wangi wakati shughuli ya utaftaji ya manowari KRI Nanggala-402 iliyopotea katika mkoa wa Java Mashariki, Indonesia, inaendelea, Aprili 25, 2021.
KRI Singa-651, meli ya kikosi cha majini cha Indonesia ikiondoka bandari ya Tanjung Wangi wakati shughuli ya utaftaji ya manowari KRI Nanggala-402 iliyopotea katika mkoa wa Java Mashariki, Indonesia, inaendelea, Aprili 25, 2021. REUTERS - AJENG DINAR ULFIANA
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Wanamaji la Indonesia limesema limetuma helikopta na meli maalum katika shughuli ya utaftaji katika eneo ambalo manowari ya KRI Nanggala-402 ilipoteza mawasiliano siku ya Jumatano, ilipokuwa ikijiandaa kwa mazoezi ya kijeshi.

Australia pia imetumia meli kubwa iliyosheheni helikopta na vifa vingine vingi kusaidia katika shughuli ya utaftaji, wakati meli ya uokoaji kwenye maji ya kina iko njiani kutoka India, huku kukiwa na wasiwasi mkuwa juu ya uwezekano wa kwamba manowari ilizamishwa n kuharibiwa vibaya na nguvu kubwa ya maji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.