Pata taarifa kuu
TAIWAN

Hamsini waangamia katika ajali ya treni Taiwan

Watu zaidi ya 50 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 60 wamejeruhiwa, baada ya treni ya abiria iliyokuwa na watu karibu watu 500 kutoka relini na kuanguka wakati treni hiyo ilikuwa ikilekea mjini Taitung.

Maafisa wa idara ya dharura nchini Taiwan wakiwa katika eneo la ajali ya treni Aprili 2, 2021.
Maafisa wa idara ya dharura nchini Taiwan wakiwa katika eneo la ajali ya treni Aprili 2, 2021. REUTERS - ANN WANG
Matangazo ya kibiashara

Hii ndio ajali mbaya ya treni kuwahi kutokea katika kisiwa hicho kwa ndani ya miongo mine.

Picha katika eneo ma ajali imeonesha mabehewa yakiwa yameanfguka relini na kuhafanya juhudi za kuwaokoa abiria waliojeruhiwa kuwa ngumu.

Abiria walionekana wakiwa wameangukia baada ya ajali, huku ikibainika kuwa baadhi ya abiria walikuwa ni familia na miongoni mwa wale waliojeruhiwa ni raia wa Ufaransa na wawili wa Japan.

Vyombo vya Habari vya Taiwan, vimeripoti kuwa watu wengi walikuwa wamesimama kwenye treni hiyo, lililokuwa na abiria wengi.

Baadhi ya mabehewa pia yaligonga, lori lilikuwa pemebeni ya eneo la ujenzi na kusababisha maafa zaidi.

Ajali hiyo imetokea wakati treni hiyo ikilekea mjini Taitung kutoka mji mkuu wa Taiwan, Taipei

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.