Pata taarifa kuu
BURMA

Burma: Aung San Suu Kyi afikishwa mahakamani, UN yahofia "vita vya wenyewe kwa wenyewe"

Kiongozi wa zamani nchini Burma (Myanmar) Aung San Suu Kyi ameitishwa mahakamani Alhamisi wiki hii saa chache baada ya mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Burma kuonya juu ya hatari ya kutokea "vita vya wenyewe kwa wenyewe" na "umwagaji mkubwa wa damu" nchini humo.

Hali nchini burma inatisha na watu wameendelea kuuawa wakati maandamano yakiendelea kupinga jaribio la mapinduzi.
Hali nchini burma inatisha na watu wameendelea kuuawa wakati maandamano yakiendelea kupinga jaribio la mapinduzi. STR AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya watu 530, wakiwemo wanafunzi wengi, vijana na watoto, wameuawa na vikosi vya usalama tangu mapinduzi ya kijeshi ya Februari 1, kulingana na shirika linalotetea haki ya Wafungwa wa Kisiasa (AAPP) nchini Burma. Mamia ya watu, wanazuliwa pasipojulikana, na wengine hawajulikani walipo.

Hakuna mashtaka mapya dhidi ya Aung San Suu Kyi, Min Min Soe, wakili wa kiongozi huyo wa zamani amesema.

Vurugu dhidi ya raia zilisababisha hasira kati ya makundi 20 ya waasi kutoka makabila mbalimbali nchini Burma. Makundi mengine waliteleleza mashambulizi dhidi ya polisi na jeshi, ambavy vilijibu kwa mashambulizi ya anga.

Kuna "hatari ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika kiwango ambacho hakijawahi kutokea," alionya Christine Schraner Burgener, mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Burma katika mkutano wa faragha wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Ameliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa "kutafakari njia zote zinazowezekana (...) kuepusha maafa katika nchi hiyo ya bara la Asia". Ameyasema hayo katika mkutano huo wa dharura ulioombwa na Uingereza

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.