Pata taarifa kuu
IRAN-CHINA

Iran na China zasaini "mkataba wa ushirikiano wa kimkakati wa miaka 25"

Beijing na Tehran wametia saini mkataba kamili wa kimkakati na kiuchumi ya miaka 25 leo Jumamosi. Mambo muhimu katika mkataba huo ni uwekezaji wa unaojirudi katika sekta tofauti: uchukuzi, nishati, viwanda na huduma. Iran ni moja ya miradi muhimu "barabara mpya za Hariri" iliyozinduliwa na rais wa China Xi Jinping mnamo mwaka 2013.

Waziri wa Mambo ya nje wa Iran na mwenzake wa China huko Tehran, Machi 27, 2021.
Waziri wa Mambo ya nje wa Iran na mwenzake wa China huko Tehran, Machi 27, 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Iran na China zimekuwa zikizungumzia mkataba huu kwa miaka kadhaa sasa. Beijing na Tehran wametia saini tu mkataba wa miaka 25 wa kimkakati na kiuchumi.

Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China, ameanzia ziara yake Mashariki ya Kati huko Riyadh na Ankara. Waziri huyo wa Mambo ya nje hakutaka kupoteza fursa hiyo na kuzuia kuahirishwa upya kwa ushirikiano huu kamili kati ya China na Iran uliozinduliwa wakati wa ziara ya Xi Jinping huko Tehran mnamo mwezi Januari 2016. Baadhi ya mambo yalivuja kwa vyomvo vya habari mnamo mwezi Juni 2020, na kusababisha sintofahamu katika ukanda huo.

Iran na China kunufaika kwa mkataba

Mkataba huu ni muhimu kwa utawala wa Iran unaokabiliwa na vikwazo vya Marekani, lakini pia kwa Beijing, ambayo imeifanya Iran kuwa hatua muhimu katika "kukarabati upya barabara ya Hariri" 9njia ya reli) kama lilivyoandika shirika la habari la China miaka mitano iliyopita. Wakati huo ndipo treni ya kwanza ya mizigo ya China iliondoka kuelekea soko la Iran, ikiwa imesheheni hasa simu za rununu, vifaa vya magari na vifaa vingine muhimu.

Mnamo mwezi Julai mwaka uliyopita, Gazeti la New York Times lilibaini kwamba Beijing ilikuwa tayari kuwekeza dola bilioni 400 katika kipindi cha miaka 25 katika sekta ya barabara, bandari, lakini pia mawasiliano ya simu, usalama wa mtandao na hata kemikali. Kwa kubadilishana, Tehran ingelifanya punguzo la 30% kwa bei ya mafuta iliyouzwa Beijing. Habari ambayo haijathibitishwa hadi leo, kwa mujibu wa Olivier Rogez, wa kitengo cha Uchumi cha RFI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.