Pata taarifa kuu
INDIA

India: Sita waangamia katika kisa cha moto katika hospitali ya Bombay

Takriban watu sita wamefariki dunia baada ya moto kuteketeza jengo moja la biashara kunakopatikana hospitali, vmamlaka katika jimbo la Mumbai, nchini India wamesema leo Ijumaa.

Moto wazuka katika lengo la biashara Bombay, India, ambako kunapatikana hopitali ya wagonjwa wa COVID-19, Machi 26, 2021.
Moto wazuka katika lengo la biashara Bombay, India, ambako kunapatikana hopitali ya wagonjwa wa COVID-19, Machi 26, 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wagonjwa 70 waliambukiwza virusi  vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa COVID-19 wamehamishiwa katika hospitali zingine, afisa mmoja amesema, akiongeza kuwa uchunguzi wa kubaini sababu za tukio hilo umeanzishwa.

Haikufahamika mara moja ikiwa wagonjwa waliotibiwa COVID-19 walikuwa miongoni mwa wahanga.

Bombay ilirekodi zaidi ya kesi 5,500 Alhamisi wiki hii, rekodi kwa hilo tangu kuzuka kwa ugonjwa huo.

Idadi ya visa vya maambukizi yapindukia milioni 11.85

India imerekodi kesi mpya 59,118 za maambukizi ya virusi vya Corona kwa siku moja, ikiwa ni idadi kubwa zaidi tangu Oktoba 18, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Ijumaa na Wizara ya Afya ya India.

Idadi ya visa vya maambukizi tangu kuzuka kwa janga hilo imefikia milioni 11.85.

India imerekodi vifo 257 kutokana na janga la COVID-19 leo Ijumaa, na kufanya jumla vifo kufikia 160,949.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.