Pata taarifa kuu
CHINA-URUSI

Urusi na China zataka mkutano wa kilele wa UN

Urusi na China zimeomba mkutano wa kilele wa wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati  kukiongezeka mvutano mkubwa wa kisiasa, huku Moscow ikisema Marekani inafanya uharibifu.

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. AP - Craig Ruttle
Matangazo ya kibiashara

Washirika hao wawili, ambao uhusiano wao na Magharibi unazidi kuharibika, walitoa wito huo katika taarifa ya pamoja baada ya mazungumzo kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili.

"Wakati mvutano wa kisiasa ukiongezeka duniani, mkutano wa wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unahitajika sana kuanzisha mazungumzo ya moja kwa moja kuhusu njia za kutatua maswala ya msingi ya yanamyozunguka binadamu kwa mlengo la kudumisha utulivu duniani," ilisema taarifa hiyo, iliyowekwa kwenye tovuti ya Wizara ya Mambo ya nje ya Urusi.

Kwa muda mrefu Moscow imekuwa ikifanya kampeni moja kwa moja kuhusu mkutano huo.

Marekani haikutajwa hasa katika taarifa hii, lakini kulingana na shirika la habari la TASS Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amesema baada ya mazungumzo na mwenzake wa China Wang Yi kwamba Moscow wala Beijing hawafurahishwi na tabia ya Marekani.

Kulingana na TASS, Lavrov amesema Washington ilikuwa ikitegemea muungano wa kijeshi na wa kisiasa wa enzi za vita baridi katika jaribio la kuharibu mfumo wa sheria za kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.