Pata taarifa kuu
MYANMAR

UN yatafuta ushahidi wa uhalifu unaofanywa na jeshi Myanmar

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa raia wa Myanmar (Burma) kukusanya na kuweka ushahidi wa uhalifu unaotekelezwa na jeshi tangu mapinduzi ya Februari 1, ili kutengeneza kesi za baadaye dhidi viongozi wake.

Waandamanaji waendelea kulengwa na vikosi vya usalama na ulinzi Myanmar.
Waandamanaji waendelea kulengwa na vikosi vya usalama na ulinzi Myanmar. DAWEI WATCH via REUTERS - DAWEI WATCH
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya waandamanaji 180 wameuawa na vikosi vya usalama tangu kuanza kwa maandamano ya amani katika nchi hiyo ya Kusini mashariki mwa Asia, Chama cha kinachotoa huduma kwa Wafungwa wa Kisiasa (AAPP) kilisema Jumatatu.

"Watu [...] wanaohusika na uhalifu mkubwa zaidi wa kimataifa kwa jumla wanashikilia nafasi za juu  katika uongozi wa nchi" na "hawaonekani hata mahali ambapo uhalifu huo unafanywa," amesema Nicholas Koumjian, mkuu wa timu ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa, katika taarifa kwa waandishi wa habari.

"Ili kuthibitisha kuhusika kwao, kunahitajika vithibitisho vya ripoti zilizopokelewa, maagizo yaliyotolewa," ameongeza.

Wale walio na habari kama hiyo wanapaswa kuwasiliana na wachunguzi kupitia njia salama za mawasiliano, amebaini, huku akitaja programu kama Signal au njia rahisi na salama ya barua pepe ya ProtonMail.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.