Pata taarifa kuu
IRAN

Suala la mpango wa nyuklia wa Iran layatia tumbo joto mataifa mbalimbali

Viongozi kutoka nchi za Magharibi wanaendelea kukutana katika jaribio la kuokoa makubaliano ya nyuklia ya Iran.

Kiongozi wa kiroho wa Iran  Ayatollah Ali Khamene.
Kiongozi wa kiroho wa Iran Ayatollah Ali Khamene. REUTERS/Khamenei.ir/Handout
Matangazo ya kibiashara

Alhamisi hii, Februari 18, Waziri wa Mambo ya nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, atawapokea kwa mazungumzo mawaziri wa mambo ya njee kutoka Uingereza na Ujerumani.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani pia atashiriki katika mkutano huo kwa njia ya video. Siku ya Ijumaa wakuu wa nchi hizi watajadili kuhusu la Iran katika mkutano wa Munich kuhusu usalama, mkutano ambao utafanyika kwa njia ya video. Lengo ni kujaribu kuokoa mkataba kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Tangu aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump kuiondoa Marekani kwenye mkataba wa mpango wa nyuklia wa Iran mnamo mwaka 2018, mivutano imekua ikiendelea kuongezeka kila kukicha.

Marekani iliamua kurejesha vikwazo kadhaa dhidi ya Iran na Tehran kutangaza kwamba inaanza tena shughuli zake za kurutubisha uranium.

Nchi za Ulaya ambazo zilitia saini kwenye mkataba wa mpango wa nyuklia wa Iran wamekuwa wakijaribu kuokoa mkataba huo tangu wakati huo.

Baada ya ushindi wa Joe Biden wengi wana matumaini kuwa mkataba huo utaokolewa baada ya sera ya "shinikizo kubwa" iliyotekelezwa na mtangulizi wake.

Utawala wa Biden umesema uko tayari kurudi kwenye mkataba huo ikiwa Tehran itatii masharti yake na kukubali tena mfumo wa mpango wake wa nyuklia.

Lakini serikali ya Iran inataka kuondolewa vikwazo kwanza kabla ya mazungumzo yoyote na kukataa wito wa kuongeza muda wa kwa mkataba huo.

Kiongozi Mkuu wa Iran Ali Khamenei alionya siku ya Jumatano (Februari 17) kwamba anataka "vitendo, sio maneno na ahadi."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.