Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-KOREA KUSINI

Korea Kaskazini: Kim Jong-un afafanua sera yake kwa Korea Kusini

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameelezea sera ambayo chama chake kinapaswa kufuata katika uhusiano na Korea Kusini, shirika la habari la serikali, KCNA limesema leo Jumatano.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un azungumza wakati wa Mkutano wa 19 wa kamati ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya 7 ya WPK;
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un azungumza wakati wa Mkutano wa 19 wa kamati ya Kisiasa ya Kamati Kuu ya 7 ya WPK; REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kim Jong-un, mwezi uliopita, alitoa wito wa kuongezewa uwezo wa kijeshi na kusema Marekani inaendelea kuwa "adui mkubwa" wa Korea Kaskazini.

Kim Jong-un, katibu mkuu wa chama tawala, alifafanua mpango wake wa sera ya miaka mitano wakati wa siku ya pili ya mikutano.

"Katibu mkuu ameonyesha majukumu ambayo jeshi la wananchi na tasnia ya makombora litalazimika kutekeleza mwaka huu," KCNA imetangaza. "Amebainisha mwelekeo unaopaswa kufuatwa na sekta inayosimamia maswala na Korea Kusini na sekta inayosimamia mambo ya nje."

Mapema mwaka huu, Kim Jong-un alikosoa vikali Seoul kwa kutoa ushirikiano juu ya "mambo yasiyokuwa muhimu", kama ugonjwa wa COVID-19 na utalii, na amependekeza kwamba Korea Kusini iache kununua silaha na kufanya mazoezi ya kijeshi na Marekani.

KCNA haikutoa maelezo zaidi juu ya mikutano ya chama tawala inayoendelea lakini imesema itaendelea kwa angalau siku ya tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.