Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI

Kim akiri "makosa" akifungua mkutano wa chama tawala

Korea Kaskazini imefungua mkutano wake wa pili wa chama tawala tangu Kim Jong-un achukue aingie madarakani katika nchi hiyo ya Kikomunisti.

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ni mkutano wa nane tu tangu kuanzishwa kwa nchi hiyo, na unakuja wiki mbili kabla ya Joe Biden kuingia madarakani. Hafla hii inaweza kufafanua sera za kiuchumi na kimataifa kwa miaka mitano ijayo.

Kim Jong-Un amekubali "makosa" katika utekelezaji wa mkakati uliopita wa miaka mitano juu ya maendeleo ya uchumi. Kufungwa kwa mipaka na jirani yake China na mshirika mkuu katika sekta ya uchumi, na vile vile mafuriko yalichangia katika urasibu mbaya wa uchumi.

Hata hivyo Kiongozi wa Korea Kaskazini ameelezea miaka mitano iliyopita kama isiyokuwa ya kawaida, na ni miongoni mwa miaka mibaya zaidi kwa nchi hiyo.

Lakini kujitosheleza bado inaonekana kuwa lengo la Pyongyang, kama alivyosema Kim Jong-un katika hotuba yake ambapo pia amesisitiza juu ya mafanikio ya Chama na uwepo na umoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.