Pata taarifa kuu
AUSTRALIA

Australia: Serikali kupinga mikataba na nchi za kigeni

Bunge la Australia limepitisha leo alhamisi muswada unaoruhusu serikali ya shirikisho kupiga kura ya turufu mikataba yoyote iliyofikiwa na majimbo ya Australia, Halmashauri za miji au taasisi za nchi hiyo za nchi za kigeni.

Waandamanaji nchini Australia wamekuwa wakipinga Serikali kuhusu inavyoshughulikia masuala ya tabia nchi na mikataba
Waandamanaji nchini Australia wamekuwa wakipinga Serikali kuhusu inavyoshughulikia masuala ya tabia nchi na mikataba Tammy Gill
Matangazo ya kibiashara

Wadadisi wanabaini kwamba hatua ya Bunge la Australia haitaifurahisha China, nchi mbili ambazo zinaendelea kuwa na mvutano.

 

Akizungumza na waandishi wa habari huko Canberra, Waziri Mkuu wa Australia, Scott Morrison, amehakikisha kwamba sheria hiyo mpya hailengi nchi yoyote, wakati wachambuzi wanaiona kama hatua inayolenga China.

 

Kulingana na nakala hiyo, Wizara ya Mambo ya nje ya Australia inaweza kupinga mikataba yoyote na serikali za kigeni ikiwa mikataba hiyo "itaathiri" uhusiano wa kigeni wa Australia na kupingana na sera ya mambo ya nje ya nchi hiyo.

 

Mkataba wennye utata uliyofikiwa mnamo mwaka wa 2018 kati ya Jimbo la Victoria na China katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya New Silk unaonekana kulengwa. Scott Morrison, ambaye alisema hapo awali kuwa mpango huo unadhoofisha uwezo wa serikali ya shirikisho kudhibiti sera za kigeni, amekataa kusema ikiwa kura ya turufu itapingwa.

 

Uhusiano kati ya Australia na China, mshirika wake mkuu wa kibiashara, umedorora tangu serikali ya Canberra ilipotaka uchunguzi wa kimataifa juu ya chanzo cha janga la Corona.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.