Pata taarifa kuu
HONG KONG-USALAMA-UCHUMI

Hong Kong: Lam kuzuru Beijing kujadili kuhusu kufufua uchumi

Kiongozi wa serikali ya Hong Kong, Carrie Lam, anatarajia kuzuru Beijing wiki ijayo kwa ziara ya siku tatu kujadili mipango ya kufufua uchumi wa kituo cha kifedha cha ulimwengu (Hong Kong), ambacho kimedhoofishwa na janga la COVID-19 na maandamano dhidi ya serikali.

Kiongozi wa serikali ya Hong Kong Carrie Lam katika mkutano na vyommbo vya habari, Julai 31,2020.
Kiongozi wa serikali ya Hong Kong Carrie Lam katika mkutano na vyommbo vya habari, Julai 31,2020. REUTERS/Lam Yik
Matangazo ya kibiashara

"Ziara yangu huko Beijing itahusu tu hali ya uchumi, ikizingatiwa hali ambayo ni mbaya sana Hong Kong," Carrie Lam amesema katika mkutano wake wa kila wiki na waandishi wa habari.

Mapema mwezi huu, Carrie Lam aliahirisha hotuba yake ya kisiasa ya kila mwaka na kuamua kufanya ziara katika kanda hiyo kujadili jinsi serikali kuu ya Beijin inaweza kusaidia kufufua uchumi wa koloni la zamani la Uingereza.

Carrie Lam ametangaza kuwa anapangilia kutoa hotuba yake mwishoni mwa mwezi wa Novemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.