Pata taarifa kuu
URUSI-NATO-NAVALNY-USALAMA-HAKI

NATO yatoa wito kwa Urusi kutoa mwanga juu ya sumu aliyopewa Alexey Navalny

Baada ya Ujerumani kutangaza kwamba kiongozi wa upinzani nchini Urusi na mkosoaji mkubwa wa rais Vladimr Putin, Alexei Navalny alipewe sumu aina ya Novichok, hali ya mvutano imeongezeka kati ya nchi za "Magharibi" na Moscow.

Alexei Navalny akishiriki katika maandamano ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kiongozi wa upinzani Boris Nemtsov huko Moscow Februari 29, 2020.
Alexei Navalny akishiriki katika maandamano ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kiongozi wa upinzani Boris Nemtsov huko Moscow Februari 29, 2020. AP Photo/Pavel Golovkin
Matangazo ya kibiashara

Hali hii inaonyesha kuepo kwa vita vipya baridi. Umoja wa Ulaya unalaani kitendo cha kupewa sumu kiongozi wa upinzani nchini Urusi na Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO, ilifanya mkutano wa dharura Ijumaa (Septemba 4) kuhusu kesi hiyo.

NATO inaitaka Urusi kuweka wazi mpango wake kamili wa Novichok.

Ujerumani iliwasilisha ushahidi usiopingika kwa washirika wake 29 wa NATO Ijumaa (Septemba 4) kuonyesha kwamba Alexei Navalny alipewa sumu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi, NATO, Jens Stoltenberg ameitaka Urusi kutoa mwanga juu ya sumu aliyopewa kiongozi huyo wa upinzani nchini Urusi. Amesema Urusi Urusi ishirikiane kikamilifu na uchunguzi usioegemea upande wowote utakaoongozwa na Shirika la kudhibiti matumizi ya silaha za sumu OPCW kuhusiana na kulishwa sumu aina ya Novitchok kwa kiongozi wa upinzani Alexei Navalny.

Kwa sasa, NATO haijatangaza hatua zozote dhidi ya Urusi. Lakini baadhi ya wajumbe wa muungano huo tayari wanafikiria uwezekano wa kufukuzwa kwa wanadiplomasia kutoka ujumbe wa Urusi kwenye jumuiya hiyo, kama baada ya Urusi kuchukuwa hatua ya kuiweka Crimea kwenye himaya yake mwaka 2014, kisha baada ya Sergei Skripal na binti yake Yulia kupewa sumu mwaka 2018 nchini Uingereza.

Katibu Mkuu wa NATO ameomba uchunguzi wa kimataifa usiopendelea upande wowote, akipinga madai ya Umoja wa Ulaya, ingawa umoja huo unakiri kwamba Urusi ina rekodi mbaya katika uchunguzi wa mashambulio dhidi ya wapinzani wake.

Stoltenberg ameongeza kwamba wanachama wa NATO sasa wanakubaliana kwamba Urusi ina maswali mazito ya kujibu. Ameyasema haya baada ya mkutano wa muungano huo uliofanyika mjini Brussels.

Lithuania imetaka kesi hiyo ijadiliwe na nchi 27 wanachama wa umoja wa Ulaya katika mkutano ujao wa EU katika wiki tatu zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.