Pata taarifa kuu
BELARUS-MAANDAMANO-SIASA-USALAMA

Belarus: Lukashenko aahidi uchaguzi mpya baada ya katiba kurekebishwa

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko ameahidi kwamba uchaguzi mpya wa urais utafanyika baada ya marekebisho ya katiba, shirika la habari la RIA limeripoti.

Maandamano yameongezeka nchini Belarus ili kumshinikiza rais Lukashenko aachie ngazi.
Maandamano yameongezeka nchini Belarus ili kumshinikiza rais Lukashenko aachie ngazi. REUTERS/David W. Cerny
Matangazo ya kibiashara

Rais Alexander Lukashenko, ambaye ushindi wake katika uchaguzi wa urais wa hivi karibuni umeendelea kuzua maandamano makubwa, saa chache zilizopita alikuwa amefutilia mbali uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi mpya wa urais.

Wakati huo huo rais wa Marekani Donald Trump amesema 'anafuatilia kwa karibu' hali inayoendelea nchini Belarus , ambapo Rais Alexander Lukashenko anaendelea kupata shinikizo la kujiuzulu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 9.

Washington tayari imetoa wito wa kuheshimu "uhuru" wa waandamanaji katika jamhuri ya zamani ya Soviet na kuitaka serikali kufanya mazungumzo na mashirika ya kiraia.

"Hii ni hali mbaya," Bwana Trump amesema alipokuwa akihojiwa kutoka bustani ya White House kabla ya kuondoka kwenda Minnesota na Wisconsin.

"Tutafuatilia kwa karibu hali inayoendelea nchini Belarus", rais wa Marekani ameongeza, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Umoja wa Ulaya unaendelea kutiwa wasiwasi na hali inayoendelea nchini Belarus.

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Charles Michel, ameitisha mkutano wa kilele wa nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya, utakaofanyika Jumatano Agosti 19 ili kujadili hali inayoendelea nchini Belarusi.

"Raia wa Belarus wana haki ya kuamua mustakabali wao na kumchague kiongozi wao kwa uhuru. Kitendo cha kuwanyanyasa waandamanaji hakikubaliki na hakiwezi kuvumiliwa, "Charles Michel ameandika kwenye kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Maandamano yameongezeka nchini Belarus ili kumshinikiza rais Lukashenko aachie ngazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.