Pata taarifa kuu
HONG KONG-MAANDAMANO-USALAMA

Wanafunzi wa shule za upili waandamana Hong Kong

Wakati China inajiandaa, Oktoba 1, kusherehekea maadhimisho ya miaka 70 ya nchi hiyo kuasisiwa, maandamano makubwa wakati mwengine yenye machafuko yalishuhudiwa mwishoni mwa wiki hii iliyopita Hong Kong.

Mmoja wa wandamanaji wanaounga mkono demokrasia akamatwa wakati wa maandamano Hong Kong, Septemba 29, 2019.
Mmoja wa wandamanaji wanaounga mkono demokrasia akamatwa wakati wa maandamano Hong Kong, Septemba 29, 2019. REUTERS/Jorge Silva
Matangazo ya kibiashara

Leo Jumatatu, Septemba 30, wanafunzi wa shule za upili wanatarajia kuingia katika mitaa mbalimbali kujiunga na wenzao katika maandamano yanayoendelea nchini humo.

Maandamano haya ya wanafunzi wa shule za upili ni kama jaribio la mwisho, kwani Jumanne wiki hii maandamano makubwa ya yanatarajiwa katika nchi hiyo.

"Mgomo dhidi ya udhalimu" ni kauli mbiu ya wanafunzi wa shule za upili ambao wanakusanyika karibu na eneo moja katikati mwa Hong Kong. Wanafunzi hao wamevaalia sare ya shule. Wameondoka madarasani Jumatatu hii asubuhi na wanatarajia kujiunga na wengine katika maandamano.

Wanasema kwamba Hong Kong ilikuwa eneo la kidemokrasia kabla ya 1997, kabla ya kuunganishwa na China, na kubaini kwamba kama wanaandamana, ni kutaka kurejesha haki zao, haki ambazo wanaamini Beijing ivunja kwa miaka kadhaa.

Wanafunzi hawa wa shule za upili wanasema: hawataki kuishi katika nchi ambayo polisi wanafikiria wana nguvu zote. Wanaomba, kama watu wengi Hong Kong, uchunguzi huru na wa haki na polisi wanaokosa wachukuliwe vikwazo.

Mamlaka  Hong Kong imekanusha taarifa zinazoishtumu polisi kwa ukandamizaji wa kikatili dhidi ya waandamanaji.
Mamlaka Hong Kong imekanusha taarifa zinazoishtumu polisi kwa ukandamizaji wa kikatili dhidi ya waandamanaji. Reuters

Vurugu kali zilizuka kati ya waandamanaji na polisi mjini Hong Kong jana Jumapili, baada ya maelfu ya watu kuandamana katika mji huo, siku ambayo maandamano kama hayo pia yaliitishwa sehemu mbalimbali ulimwenguni, kuwaunga mkono raia wa Hong Kong kwa lengo la kuchafua sifa ya maadhimisho ya miaka 70 ya China tangu ilipoundwa kuwa Jamhuri ya watu wa China.

Maadhimisho hayo makubwa yatakayofanyika siku ya Jumanne yatahusisha gwaride kubwa la kijeshi ambayo yataashiria kuibuka kwa nchi hiyo kama taifa lenye nguvu kubwa ulimwenguni.

Hong Kong ambayo ina utawala wa ndani imekumbwa na ghadhabu ya umma kufuatia utawala wa China kukandamiza haki zao maalum. Wanaharakati wanaotetea demokrasia Hong Kong wameapa kuimarisha maandamano yao kupinga utawala wa kiimla, kuelekea siku ya Jumanne ya sherehe za China.

Vurugu zakumba maandamano Hong Kong kuelekea maadhimisho ya miaka 70 ya China kuasisiwa.

Vurugu kali zilizuka kati ya waandamanaji na polisi mjini Hong Kong ljana, baada ya maelfu ya watu kuandamana katika mji huo, siku ambayo maandamano kama hayo pia yameitishwa sehemu mbalimbali ulimwenguni, kuwaunga mkono Wahong Kong kwa lengo la kuchafua sifa ya maadhimisho ya miaka 70 ya China tangu ilipoundwa kuwa Jamhuri ya watu wa China. Maadhimisho hayo makubwa yatakayofanyika siku ya Jumanne yatahusisha gwaride kubwa la kijeshi ambayo yataashiria kuibuka kwa nchi hiyo kama taifa lenye nguvu kubwa ulimwenguni. Lakini ukamataji wa waandamanaji unaoendelea Hong Kong unatishia kuvuruga maadhimisho hayo.

Hong Kong ambayo ina utawala wa ndani imekumbwa na ghadhabu ya umma kufuatia utawala wa China kukandamiza haki zao maalum. Wanaharakati wanaotetea demokrasia Hong Kong wameapa kuimarisha maandamano yao kupinga utawala wa kiimla, kuelekea siku ya Jumanne ya sherehe za China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.