Pata taarifa kuu
IRAN-MAREKANI-NYUKLIA-USALAMA

Iran yasitisha baadhi ya ahadi zake kwa mpango wa nyuklia

Iran imetangaza Jumatano wiki hii kwamba itasitisha kutekeleza "baadhi" ya "ahadi zake" ilizotoa katika mfumo wa makubaliano ya kimataifa juu ya mpango wake wa nyuklia wa mwaka 2015, kufutia hatua ya Marekani ya kujiondoa kwenye mkataba huo.

Rais wa Iran Hassan Rohani na mkurugenzi wa shirika la Nishati ya Nyuklia ya Iran Ali Akbar Salehi wakati wa kuadhimishwa siku ya Nishati ya Nyuklia Aprili 9, 2019, Tehran.
Rais wa Iran Hassan Rohani na mkurugenzi wa shirika la Nishati ya Nyuklia ya Iran Ali Akbar Salehi wakati wa kuadhimishwa siku ya Nishati ya Nyuklia Aprili 9, 2019, Tehran. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo linakuja wakati mvutano unaendelea kuongezeka kati ya Iran na Marekani, ambayo ilitangaza Jumanne wiki hii kuwa imetuma ndege za kivita za B-52 katika eneo la Ghuba.

Washington inaichulia Iran kama adui yake namba moja Mashariki ya Kati na Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ambaye alizuru Baghdad Jumanne aliishtumu Iran kwamba inaandaa "mashambulizi makubwa" dhidi ya majeshi ya Marekani.

Iran itasitisha kuzuia hifadhi zake za maji mazito na uranium, ambapo ni katika ahadi ilizotoa katika makubaliano yaliyofikiwa Vienna mwaka 2015, hali ambayo inapunguza kikamilifu mpango wake wa nyuklia, Baraza Kuu la usalama wa taifa (CSSN) limesema katika taarifa iliyochapishwa na shirika la habari la Irna.

Uamuzi huo umetangazwa rasmi mapema asubuhi, jijini Tehran, mbele ya mabalozi wa nchi zilizoshiriki kwenye mkataba huoz (Ujerumani, China, Ufaransa, Uingereza na Urusi).

Baada ya kupitishwa na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, mpango wa nyuklia wa Iran wa mwaka wa 2015 uliruhusu nchi hiyo kuondolewa sehemu ya vikwazo vya kimataifa vilivokuwa vinailenga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.