Pata taarifa kuu
SRI LANKA-USALAMA

Mashambulizi Sri Lanka: Idadi ya waliouawa yaongezeka na kufikia 290

Idadi ya waliouawa katika mashambizi ya makanisa nchini Siri Lanka imeongezeka na kufikia 290. Wakati huo huo watu kumi na tatu wamekamatwa kuhusiana na mashambulizi hayo, kwa mujibu wa polisi.

Mashambulizi nchini Sri Lanka: Katika eneo la kanisa la St SebastianNegambo, mojawapo ya makanisa na hoteli zilizokumbwa na milipuko, polisi inaendelea na uchunguzi, Aprili 22, 2019.
Mashambulizi nchini Sri Lanka: Katika eneo la kanisa la St SebastianNegambo, mojawapo ya makanisa na hoteli zilizokumbwa na milipuko, polisi inaendelea na uchunguzi, Aprili 22, 2019. REUTERS/Athit Perawongmetha
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya 500 wamejeruhiwa. Milipuko minane iliripotiwa katika mashambulio dhidi ya makanisa matatu mjini Kochchikade, Negombo na Batticaloa ambayo yalisahambuliwa wakati wa ibada ya Pasaka jana Jumapili.

Kumekua na hofu huenda wapiganaji wa kundi la Islamic State waliorejea kutoka mashariki ya kati wakawa tishio kwa usalama wa nchi hiyo.

Pia kumeripotiwa idadi kubwa ya watu waliyojeruhiwa katika kanisa la St Anthony mjini Kochchikade, ambao ni moja ya wilaya ya Colombo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.