Uchaguzi wa urais Indonesia: Widodo aongoza lkwa kura nyingi
Rais anaye maliza muda wake nchini Indonesia, Joko Widodo, anaonekana kuwa atashinda uchaguzi wa urais uliyofanyika leo Jumatano Aprili 17, 2019.
Imechapishwa:
Joko widodo anaongoza kwa 54.7% ya kura hadi 55.7% kupitia mfumo wa kuhesabu haraka kwa jumla ya 55% hadi 78 ya kura ambazo zimekwisha hesabiwa.
Hata hivyo, Philips Vermonte, Mkurugenzi wa taasisi ya CSIS, inayofuatilia kwa karibu uchaguzi huo, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba ni mapema kutangaza mshindi wa uchaguzi huo.
Kambi ya Prabowo pia imetoa wito kwa wafuasi wake kuwa na uvumilivu. "Tutasubiri," amesema msemaji wa kampeni ya Prabowo Subianto, Dahnil Anzar Simanjuntak, akibainisha kwamba bado ni mapema kumjuwa mshindi.
Zaidi ya raia milioni 192 wa Indonesia wamepiga kura Jumatano hii kumchagua rais wao na wabunge baada ya kampeni iliyodumu miezi sita, ambayo ilitawaliwa na masuala ya kiuchumi na kuongezeka kwa ushawishi wa Uislam wa kihafidhina.