Korea Kaskazini yawarudisha nyumbani maafisa wake kutoka mpakani
Korea Kaskazini imeondoa maafisa wake katika Ofisi pamoja na jirani yake Korea Kusini, iliyofunguliwa mwaka uliopita kwa lengo la kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Imechapishwa:
Wizara ya Ushirikiano wa nchi hizo mbili za Korea , imesema, imepata taarifa Ijumaa asubuhi kuwa maafisa wa Korea Kaskazini wataondoka baadaye Ijumaa.
Korea Kusini imesikutishwa na uamuzi huo wa Pyongyang na kutoa wito kwa maafisa hao kurejea tena haraka iwezekanavyo ili kuendeleza ushirikiano huo.
Maafisa wa juu wa Korea Kaskazini na Kusini, hawajakutana tangu kumalizika bila mwafaka kati ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na rais wa Marekani Donald Trump waliokutana mwezi uliopita.