Pata taarifa kuu
JAPAN-GHOSN-UCHUMI-HAKI

Japan: Mahakama yafutulia mbali ombi la kuongezwa muda wa kuzuiliwa Carlos Ghosn

Mahakama ya Japan imetangaza leo Alhamisi kwamba imekataa ombi jipya la kuongezwa muda wa kuzuiliwa Carlos Ghosn. Kulingana na vyombo vya habari vya Japan, Mwenyekiti bodi ya wakurugenzi ya Renault na muungano wa Renault-Nissan anaweza kuachiliwa huru kwa dhamana hivi karibuni.

Eneo anakozuiliwa Carlos Ghosn.
Eneo anakozuiliwa Carlos Ghosn. REUTERS/Issei Kato
Matangazo ya kibiashara

Ghosn na mshirika wake wa karibu Greg Kelly, walikamatwa na kuwekwa nchini ya ulinzi wa polisi Novemba 19. Kwa mujibu wa kituo cha habari cha serikali NHK, Carlos Ghosn anaweza kuachiliwa huru Ijumaa wiki hii baada ya kutoa dhamana, kwa kusubiri kesi yake, kwa mujibu wa shirika la Habari la AFP.

Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya kuunda magari ya Nissan nchini Japan Carlos Ghosn ameshtakiwa kwa kuficha mapato kwa kipindi cha miaka mitano. Carlos Ghosn yuko mikononi mwa vyombo vya sheria vya Japan tangu mwezi Novemba mwaka huu, akidaiwa kuhusika na tuhuma mbaya ya matumizi ya fedha za mwajiri wake.

Carlos Ghosn, mwenye umri wa miaka 64, mbali na kuwa mwenyekiti wa Nissan, pia ana wadhifa kama huo katika kampuni ya magari ya Mitsubishi na Mtendaji Mkuu wa kambuni ya magari ya Renault.

Miongoni mwa tuhuma zinazomkabli, ni kupotosha mshahara wake akidai anapokea pungufu na wakati huo huo akitumia mali ya kampuni kwa manufaa binafsi.

Kwa mujibu wa vyanzo vilio karibu ya kesi hiyo, Ghosn akiwa na mtendaji mwingine, Gerg Kelly, walikula njama kuanzia mwaka 2010 kufanya malipo ya fidia.

Kulingana na sheria za Japan, iwapo Ghosn atapatikana na hatia ya kughushi taarifa za kiusalama anaweza kuingia jela miaka 10, au kulipa faini ya Yen milioni 10.

Kushikiliwa kwa gwiji huyo kwenye nafasi nyeti katika kampuni za magari, kumeleta mtikisiko katika sekta nzima ya uundaji wa magari

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.