Pata taarifa kuu
KOREA KAKAZINI-KOREA KUSINI-USHIRIKIANO

Seoul na Pyongyang kuzungumza kabla ya mkutano wa marais

Wawakilishi kutoka Seoul na Pyongyang wanakutana Jumatatu wiki hii kwa mazungumzo ya ngazi ya juu, kabla ya mkutano kati ya viongozi wa pande zote mbili za rasi ya Korea, gazeti la kila siku la Korea Kusini la Kookmin Ilbo limeripoti.

Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wakisabahiana baada ya kumalizi kwa mkutano wao wa kihistoria katika jiji la Panmunjom, Korea ya Kaskazini, Mei 26, 2018.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un wakisabahiana baada ya kumalizi kwa mkutano wao wa kihistoria katika jiji la Panmunjom, Korea ya Kaskazini, Mei 26, 2018. The Presidential Blue House /Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Kim Jong-un, kiongozi wa Korea Kaskazini, na Moon Jae-in, rais wa Korea Kusini, walikutana mwezi Aprili na walikubaliana kuandaa mkutano katika majira ya baridi huko Pyongyang.

Gazeti la kila siku la Kookmin Ilbo likinukuu afisa mwandamizi wa Korea Kusini, limeripoti kwamba mkutano huo unatarajiwa kufanyika kabla ya mwishoni mwa mwezi Agosti.

Msemaji wa Moon Jae-in alisema siku ya Jumapili kuwa ofisi ya rais wa Korea Kusini ina imani kuwa tarehe ya mkutano huo inaweza kujadiliwa Jumatatu wiki hii.

"Tunatarajia kuwa tarehe, eneo na wajumbe katika mkutano huo wa kihistoria vinaweza kujadiliwa leo Jumatatu," msemaji wa rais amesema bila kutoa maelezo zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.