Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI-MAREKANI-USHIRIKIANO

Korea Kaskazini yafuta mkutano na Mike Pence

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence alikuwa tayari kukutana na ujumbe wa maafisa waandamizi wa Korea Kaskazini kando ya mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi lakini hii "mkutano huo" ulifutwa «dakika za mwisho" na Pyongyang.

Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence.
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence. REUTERS/Ammar Awad
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo ulifutwa na serikali ya Korea Kaskazini baada ya kauli nzito ya Bw Pence, serikali ya Marekan imetangaza.

Maafisa wa Marekani wanasema wajumbe wa Korea Kaskazini walijiondoa ghafla kutoka kwa mkutano wa faraghani uliokuwa umepangwa kufanyika mjini Seoul, Korea Kusini saa mbili kabla ya mkutano huo kufanyika.

Wakati wa ziara ya Mike Pence katika mji wa Pyeongchang, nchini Korea Kusini, kwenye ufunguzi wa mashindano ya Olimpiki, "kulikuepo na uwezekano wa mkutano mfupi na viongozi wa ujumbe wa Korea Kaskazini," amesema Msemaji wa wizara ya mashauriano ya kigeni ya Marekani Heather Nauert.

Makamu wa Rais alikuwa tayari kuchukua fursa hii ili kuonyesha haja ya Korea ya Kaskazini kuachana na mipango yake isio halali nyuklia na majaribio ya makombora ya masafa marefu, "amesema katika taarifa yake.

"Dakika za mwisho, Maafisa wa DPRK (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea) waliamua kutoendelea na mkutano huo. Tunasikitishwa sana na kukosa kwao kutumia fursa hii," ameongeza Healther Nauert.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.