Pata taarifa kuu
KOREA KASKAZINI

Korea Kaskazini yawekewa vikwazo vipya na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Baraza la Uslama la Umoja wa Mataifa limeiwekea vikwazo vipya nchi ya Korea Kaskazini.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa 路透社
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivi ambavyo vimeungwa mkono na China ambaye ni mshirika wake karibu, vinalenga kutatiza juhudi za Pyongyang kuendelea na mradi wake wa silaha za Nyuklia.

Baraza hilo limekubaliana kuiwekea vikwazo vya usafirishaji wa mafuta, bidhaa muhimu ambayo inaaminiwa kuwa imekuwa ikisaidia sana nchi hiyo kuendelea na mradi wake.

China ambayo imekuwa msafirishaji mkubwa wa mafuta, nchini Korea Kaskazini, inasitisha huduma hiyo ambayo inalenga kuiadhibu Pyongyang.

Hili ni azimio la tatu la vikwazo dhidi ya serikali ya Korea Kaskazini mwaka 2017.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema amefurahishwa na hatua hii ambayo ameelezea kuwa ni ishara kuwa Jumuiya ya Kimataifa inataka amani.

Korea Kaskazini imeendelea kuwa tishio la usalama duniani kwa kurusha makombora yake ya masafa marefu katika eneo la Korea na kutishia usalama wa nchi jirani kama Japan na Korea Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.