Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Marekani yajenga mtambo wa kulinda Korea Kusini

Korea Kusini imesema wanajeshi wa Marekani wameanza kujenga mtambo wa kisasa wa kuzuia makombora katika eneo moja kusini mwa nchi hiyo.

Makomboya ya Korea Kaskazini aina ya «Pukkuksong»
Makomboya ya Korea Kaskazini aina ya «Pukkuksong» REUTERS/Damir Sagolj
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya ulinzi ya Korea Kusini imesema mtambo huo utakamilishwa na utakuwa tayari kutumika katika kipindi cha mwaka mmoja..

Mtambo huo wa kujilinda dhidi ya makombora, ambao hufahamika kitaalamu kama THAAD, kwa Kiingereza Terminal High Altitude Area Defense, kutokana na wasiwasi wa tishio kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo imeendelea kufanyia majaribio makombora.

Mtambo huo unajengwa katika wilaya ya Seongju. Lakini China imekuwa ikipinga kuwekwa kwa mtambo huo.

Awali rais wa Marekani Donald Trump ameashiria kwamba Marekani iko tayari kuchukua hatua kivyake bila kuishirikisha China kukabiliana na tishio la nyuklia kutoka kwa Korea Kaskazini.

Kumekuwepo na taarifa za kutokea kwa makabiliano kati ya wenyeji na polisi eneo panapojengwa mtambo huo, ambalo awali lilikuwa uwanja wa mchezo wa gofu.

Hayo yanajiri wakati ambapo rais wa Marekani anatarajiwa kukutana na Maseneta 100 wa nchi hiyo katika Ikulu ya White House kuhusu Korea Kaskazini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.