Pata taarifa kuu

Waandamanaji wamngo'oa madarakani Waziri wa Sheria Romania

Maandamano yaliyokua yakiendelea nchini Romania yamesababisha Waziri wa Sheria Florin Iordache, kujiuzulu Alhamisi hii, Februari 9. Maandamano hayo yalianza katika mji wa Bucharest tangu Februari 1.

Katika mji wa Bucharest, maandamano makubwa dhidi ya amri mbili zinazotoa mabadiliko ya sheria ya jinai nchini Romania, Jumapili, Januari 22, 2017.
Katika mji wa Bucharest, maandamano makubwa dhidi ya amri mbili zinazotoa mabadiliko ya sheria ya jinai nchini Romania, Jumapili, Januari 22, 2017. Inquam Photos/Liviu Florin Albei/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya watu waliingia mara kadhaa mitaani kupinga dhidi ya amri ya dharura iliyotolewa na serikali ili kuruhusu sera ya kutoroka gerezani kwa rushwa.

Kufuatia hali hiyo, nakala hiyo iliondolewa Februari 4, lakini haikutosha. Raia walipandwa na hasira na kupoteza imani kwa serikali ambapo waliomba serikali kujiuzulu. Tayari waandamanaji wamepata ushindi wa kwanza ikiwa ni pamoja na kujiuzulu kwa Waziri wa Sheria, Florin Iordache, mmoja wa wa viongozi waliopendekeza kuchukuliwa kwa amri hiyo.

Waziri wa Sheria wa Romania, Florin Iordache, wakati wa hotuba yake baada ya kujiuzulu kwake siku ya Alhamisi Februari 9, 2017.
Waziri wa Sheria wa Romania, Florin Iordache, wakati wa hotuba yake baada ya kujiuzulu kwake siku ya Alhamisi Februari 9, 2017. Inquam Photos/Octav Ganea/via REUTERS

Maandamano haya ya raia wa Romania yanakumbusha tukio jingine la zamani, ambalo halitosahaulika katika historia ya nchi hiyo.Mwezi Desemba 1989, serikali ya Ceausescu ilikabiliwa na maandamano makubwa katika historia ya nchi hiyo na kupelekea baadhi ya mambo kubadilika. Florina Cozigian ni miongoni mwa waandamanaji ambao walimpinga udikteta wa kikomunisti na kudai kuondoka kwa kiongozi wa utawala huo. Mumewe wakati huo alikua akihudumu nje ya nchi, lakini Florina na mtoto wao, Paul, walikwama nchini Romania. Wakifuatliwa kwa karibu, hawakupata nafasi ya kuondoka nchini kwa kumsihindikiza. Hili ni tukio ambalo Florina hatosahau katika maisha yake

Leo anaamini kwamba demokrasia si mchezo. "[Wakati wa utawala wa Ceausescu], nilikuwa mdogo Ilikuwa dhuluma kabisa. Kisha tulijikomboa na hali hiyo ilibadili mambo mengi ," Florina mesema.

"Tunatakiwa kuwa watu wenye busara na nchi yetu, ikilinganishwa na miaka hiyo iliyopita, lakini rushwa ni ugonjwa. Ni aibu kwetu, " Florina Cozigian, mwandamanaji, mwenye umri wa miaka 82, amesema

Aibu hii alioihisi Florina ilimpelekea aingiye mitaani, akiwa na umri wa miaka 82, akiwa na mtoto wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.