Pata taarifa kuu
UTURUKI-USALAMA

Mshukiwa mkuu wa mauaji ya mjini Istanbul akamatwa

Polisi nchini Uturuki imemkamata mshukiwa mkuu wa mauaji ya watu 39 akiyetekeleza shambulizi la kigaidi katika kilabu ya usiku wakati wa mkesha wa mwaka mpya.

Mbele ya makao makuu ya polisi mjini Istanbul, Januari 17, 2016.
Mbele ya makao makuu ya polisi mjini Istanbul, Januari 17, 2016. REUTERS/Osman Orsal
Matangazo ya kibiashara

Kuna picha zinatembea kwenye mtandao wa internet zikimuonyesha mtu anadaiwa kuwa ndie mshambuliaji wa klabu maaarufu jijini Istambul akivalia shati lililojaa damu, ishara ya kwamba amepewa kipigo ambae alikamatwa magharibi mwa jiji la Istambul akiwa na mwanae wa miaka minne.

Abdulgadir Masharipov ndilo jina lake, ni mzaliwa wa Uzbekistan lakini kwenye kundi linalojiita Islamic State anatumia jina la Abou Mohammad Khorassani ambae alikamatwa baada ya Operesheni katika nyumba moja ambayo mtuhumiwa alipanga kujificha ambayo hakutumia kufuatia msako uliokuwepo.

Mtuhumiwa huyo wa mashambulizi alipelekwa moja kwa moja Hospitalini kwa ajili ya vipimo vya afya. Ni mara ya kwanza nchini Uturuki mtuhumiwa wa mashambulizi ya Kigaidi ya kundi linalojiita Islamic State anakamatwa akiwa bado hai na anaweza kufikishwa kizimbani.

Alikuwa anasakwa tangu siku kumi na sita zilizopita baada ya kutekeleza mauaji dhidi ya watu waliokuwa wakisherehekea siku kuu ya mwaka mpyakatika klabu moja ya Usiku na kuwauwa watu 39 wakiwemo raia wa kigeni 27 kutoka katika nchi za Morocco, Lebanon, Saudia Arabia, Israel, na Iraq.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.