Pata taarifa kuu
JAPAN-MAREKANI-USHIRIKIANO

Waziri Mkuu wa Japan aendelea na ziara yake nchini Marekani

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe ametembelea maeneo kadhaa katika jimbo la Hawaii nchini Marekani walikouawa wanajeshi wa nchi yaka wakati wa vita vya pili vya dunia mwaka 1941.Waziri Mkuu Abe anakuwa kiongozi wa kwanza wa Japan kuzuru iliyokuwa kambi ya wanajeshi wa majini wa Marekani, wakati Japan ilipotekeleza shambulizi hilo.Rais Barrak Obama naye anazuru eneo hilo na kuwa rais wa kwanza kwenda eneo hilo kama kiongozi wa Marekani tangu mwaka 1941.Ripoti zinasema kuwa, Abe atawakumbuka wanajeshi wa nchi yake waliopoteza maisha yake lakini hataomba radhi kwa uvamizi uliofanywa dhidi ya nchi yake.Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya wanajeshi wa Marekani zaidi ya elfu mbili na kuingiza Marekani katika vita vya pili vya dunia.Marekani ililipiza kisasi bvaada ya kushambulia miji ya Japan ya Nagasaki na Hiroshima na kusababisha vifo vya maefu ya watu mwaka 1945.

Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri Mkuu wa japan Shinzo Abe, kwenye daraja la Ujibashi katika mji wa Ise, Mei 26, 2016, siku ya mkutano wa G7.
Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri Mkuu wa japan Shinzo Abe, kwenye daraja la Ujibashi katika mji wa Ise, Mei 26, 2016, siku ya mkutano wa G7. REUTERS/Toru Hanai
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Abe anakuwa kiongozi wa kwanza wa Japan kuzuru iliyokuwa kambi ya wanajeshi wa majini wa Marekani, wakati Japan ilipotekeleza shambulizi lake.

Rais Barak Obama naye anazuru eneo hilo na kuwa rais wa kwanza kwenda eneo hilo kama kiongozi wa Marekani tangu mwaka 1941.

Ripoti zinasema kuwa, Abe atawakumbuka wanajeshi wa nchi yake waliopoteza maisha lakini hataomba radhi kwa uvamizi uliofanywa dhidi ya nchi yake.

Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya wanajeshi wa Marekani zaidi ya elfu mbili na kuingiza Marekani katika vita vya pili vya dunia.

Marekani ililipiza kisasi baada ya kushambulia miji ya Japan ya Nagasaki na Hiroshima na kusababisha vifo vya maefu ya watu mwaka 1945.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.