Pata taarifa kuu
THAILAND-USALAMA

Mtu mmoja auawa katika shambulizi kusini mwa Thailand

Mtu mmoja ameuawa na wengine thelathini wamejeruhiwa katika shambulizi la bomu lililotegwa ndani ya gari usiku wa Jumanne kuamkia Jumatatu kusini mwa Thailand, polisi imefahamisha Jumatano hii Agosti 24.

Askari polisi wa Thailand apiga doria katika mji wa Hua Hin baada ya milipuko miwili  Agosti 12.
Askari polisi wa Thailand apiga doria katika mji wa Hua Hin baada ya milipuko miwili Agosti 12. MUNIR UZ ZAMAN / APF / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hili linatokea wiki mbili baada ya mfululizo wa mashambulizi mengine yalitoendeshwa katika maeneo mengine ya mapumziko nchi humo.

Mtu aliyeuawa katika shambulizi hili ni raia wa Thailand mwenye umri wa miaka 34, ambaye alikuwa karibu na hoteli ya Southern, iliyolengwa na shambulio la bomu katika eneo linalotembelewa na watu wengi katika mji mkuu wa jimbo la Pattani. Kwa mujibu wa vyanzo hospitali, hakuna raia wa kigeni ambaye ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa, ambapo watano wako katika hali mbaya. Ka mujibu wa polisi jengo la Hoteli limeharibiwa na mlipuko huo.

Bomu la kwanza, la kiwango cha chini, lililipuka mapema nje ya baa karibu na hoteli hiyo, na kuzua hofu katika eneo hilo ambapo kuna kunapatikana baa nyingi na migahawa. Mlipuko wa bomu la pili, lililokua limewekwa katika gari ndogo, lililenga sehemu ya kuingilia katika hoteli ya Southern dakika 45 baadaye.

Pattani, moja ya majimbo matatu waasi wa Kiislamu wamekua wakiendesha harakati zao, si maeneo ya kitalii na yanavutia tu watu wachache wasio kuwa raia wa Thailand. Hata hivyo, serikali inajaribu kukuza utalii.

Mashambulizi ya mabomu yamekua yakitokea mara kwa mara katikajimbo hili, licha ya kutodaiwa na kundi lolote, lakini yamekua yakihusishwa kundi la watu wanaotaka kujitenga na utawala wa Thailand.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.