Pata taarifa kuu
INDIA-MACHAFUKO

India: watu 19 wauwawa katika vurugu za kijamii

Vurugu zinazohusiana na mfumo wa kijamii kaskazini mwa India zimesababisha watu 19 kupoteza maisha na 200 kujeruhiwa, chanzo cha serikali za mitaa kimesema.

Watu kutoka jamii ya Jatwakizungukwa na polisi wakati wa maandamano ya tarehe 21 Februari, 2016, katika mji wa New Delhi.
Watu kutoka jamii ya Jatwakizungukwa na polisi wakati wa maandamano ya tarehe 21 Februari, 2016, katika mji wa New Delhi. REUTERS/Adnan Abidi
Matangazo ya kibiashara

"Watu kumi na tisa wamekufa na zaidi ya 200 kujeruhiwa," amesema P. K. Das, afisa mwandamizi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya jimbo la Haryana, na kuongeza kuwa hali inaonekana kuwa shwari, hata hivyo.

Makabiliano makali yaiotokea Jumapili hii, Februari 21 kati ya polisi na waandamanaji katika jimbo la Haryana, karibu na New mji wa Delhi.

Watu kutoka jamii ya Jats, wakulima wanaojulikana kwa tabia za kupigana, wanaandamana kwa zaidi ya wiki moja sasa wakidai ushirikishwaji wao katika jamii za watu wasiokua na maendeleo ili waweze kupata nafasi katika utawala na vyuo vikuu.

Katika siku za hivi karibuni, walichoma vituo vya treni, kituo cha biashara nawalizuia Barabara kuu zinazoingia katika mji mkuu na moja ya vituo vikubwa kinachosambaza maji mjini New Delhi. . Awali serikali ilitangaza watu kumi na mbili ndio waliuawa

Jeshi lilitumia mabomu ya machozi ili kuwaondoa waandamanaji ambao walikuwa wamezuia kituo cha Munak Mfereji, moja ya vituo vikuu vya maji katika mji wa New Delhi. Vifaa kadhaa vimeharibiwa na 60% ya mji mkuu kwa sasa unakabiliwa na mgawo wa maji. Mgogoro huo umeilazimu serikali ya mkoa kufunga shule katika mji wa New Delhi Jumatatu hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.