Pata taarifa kuu
MYANMAR - USALAMA

Aung San Suu Kyi apewa ulinzi zaidi baada ya kitisho cha usalama wake

Aung San Suu Kyi ambae chama chake kimechukuwa uongozi wa bunge hivi karibuni nchini Myanmar, amepewa ulinzi mkali wa usalama baada ya kutolewa kwa vitisho vya kumuuwa kupitia mtandao wa kijamii wa facebook duru za polisi zimeeeleza.

Myanmar's National League for Democracy leader Aung San Suu
Myanmar's National League for Democracy leader Aung San Suu © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi mmoja wa polisi ambae hakupenda jina lake litajwe amesema usalama umeimarisha zaidi kwa kiongozi huyo.

Mshauri mmoja wa Aung San Suu Kyi ambae pia hakupenda jina lake litajwe amesema hatuwa hiyo ya ulinzi zaidi imechykuliwa kufuatia vitisho vya mtu mmoja kupitia facebook.

Mtu huyo alietowa kitisho kupitia mtandao wa facebook amekuwa akiomba radhi na ambapo tangu juma lililopita aliahidi kumkata kichwa yeyote yule ataejaribu kurekebisha katiba ili kuondowa kipengele kinacho mzuia Aung San Suu Kyi kuwa rais.

Ingawaje mtu huyo hakutaja jina la Aung San Suu Kyi, kitisho hicho kilichukuliwa kwa umakini.
Katiba ya nchi hiyo inamzuia mtu mwenye watoto wenye uraia wa kigeni kuwa rais, wakati ambapo watoto wawili wa Aung San Suu Kyi ni raia wa Uingereza.

Aung San Suu Kyi anampango wa kufanya mabadiliko ya katiba, au kumteuwa mtu wake wa karibu kupitia bunge lenye wajumbe wengi wa chama chake.

Katika mkesha wa tarehe 17 Februari tarehe ambayo jina la rais na makam wake wawili linapashwa kutangazwa, majadiliano yanaendelea chini kwa chini.

Serikali yake, ambayo ni ya kwanza kuchaguliwa kupitia misingi misingi ya kidemokrasia tangu miongo kadhaa ya uongozi wa kijeshi, inatakiwa kuanza shughuli zake Aprili Mosi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.