Pata taarifa kuu
CHINA-Maandamano-Siasa

China: wandamanaji waaendelea kupiga kambi katika barabara za Hong Kong

Waandamanaji wanaodai kutetea uwepo wa misingi ya kidemokrasia nchini China, hususan katika mji wa Hong Kong, wameendelea kupiga kambi katika barabara za mitaa mingi ya Hong Kong. Wiki moja imekamilika sasa tangu maandamano hao yaanze.

Wanafunzi wa vyuo vikuu Hong Kong wanaendelea na msimamo wao wa kumtaka Waziri Mkuu ajiuzulu, huku wakiomba kufanyike uchaguzi wenye misingi ya kidemokrasia.
Wanafunzi wa vyuo vikuu Hong Kong wanaendelea na msimamo wao wa kumtaka Waziri Mkuu ajiuzulu, huku wakiomba kufanyike uchaguzi wenye misingi ya kidemokrasia. RFI/Heike Schmidt
Matangazo ya kibiashara

Hali ya taharuki ilitanda Ijumaa wiki hii katika mitaa ya kibiashara ya Hong Kong, baada ya machafuko kutokea kati ya wanaharakati hao wanaotetea kuimariswa kwa misingi ya kidemokrasia na wapinzani wao.

Waandamanaji hao wameendelea kupiga kambi kwa muda wa wiki moja sasa katika barabara za eneo muhimu la kibiashara la Causeway Bay. Wengi miongoni mwa waandamanaji hao ni wanafunzi wa vyuo vikuu vya Hong Kong, ambao wengi wao wamekua wakilala kwenye mahema ya plastiki, huku vijana wakionekana kuwa kwenye mstari wa mbele katika maandamano hayo.

Haijajulikana iwapo makabiliano kama ya Ijumaa wiki hii yatajitokeza tena kati ya waandamanaji na wapinzani wao.

Katika eneo la kibiashara la Causeway Bay, Hong Kong.
Katika eneo la kibiashara la Causeway Bay, Hong Kong. Photo: RFI/Heike Schmidt

Katika maeneo ya kibiashara ya Causeway na Mongkok, waandamanaji wamekua wakikabiliana na kundi la watu ambao wanapinga maandamano hayo. Kundi hilo limekua likiwarushia mawe na machupa yenye maji waandamanaji likiwataka waandamanaji hao waondoke maeneo hayo ya kibiashara na waweze kujielekeza makwao.

Ijumaa wiki hii wakati wa makabiliano kati ya pande hizo mbili, polisi iliingilia kati kwa makini ili kujaribu kuzima machafuko yaliokua yakishuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya mji wa Hong Kong.

Waandamanaji wanaituhumu serikali na polisi kutumia makundi ya vijana ili kuwashambulia na kusababisha hali ya taharuki.

waandamanaji wameapa kuendelea na maandamano Hong Kong, nchini China.
waandamanaji wameapa kuendelea na maandamano Hong Kong, nchini China. Photo: RFI/Heike Schmidt

Baada ya wiki moja ya maandamanao, mazunguzo yaliyokua yameanza Ijumaa wiki kati ya waandamanaji na serikali yamegonga mwamba, huku waandamanaji wakiapa kuendelea harakati zao hadi pale serikali itasitisha mashambulizi dhidi yao. Awali waandamanaji hao walimuomba Waziri mkuu Leung Chun-ying ajiuzulu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.