Pata taarifa kuu
URUSI-UKRAINE-Usitishwaji mapigano-Usalama

Mazungumzo kati ya Vladimir Putin na Petro Porochenko yakumbwa na giza

Marais wa Ukraine na Urusi, Petro Porochenko na Vladimir Putin wamekubaliana kumaliza machafuko yanayoendelea mashariki mwa Ukraine, ikulu ya Kiev imetangaza jumatano wiki hii, baada ya marais hao kuongea kwa simu.

Wanajeshi wa Ukraine katika jimbo la Lougansk, Agosti 26 mwaka 2014.
Wanajeshi wa Ukraine katika jimbo la Lougansk, Agosti 26 mwaka 2014. REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa tangazo liliyotolewa na ikulu ya Kiev, rais wa Ukraine amezungumza kwa simu na mwenziye wa Urusi Vladimir Putin na kukabiliana kusitisha mapigano katika eneo la madini linalojumuisha majimbo ya Donetsk na Lougansk, ambako kunashuhudiwa mapigano makali kati ya jeshi na waasi wanaoungwa mkono na Urusi.

Hata hivo msemaji wa rais wa Urusi amekanusha taarifa hizo, na kubaini kwamba Urusi haihusiki katika mapigano hayo yanayoendelea mashariki mwa Ukraine.

Baada ya ya kufanya vizuri dhidi ya waasi katika wiki kadhaa zilizopita, jeshi la Ukraine limeshindwa kuyaweka kwenye himaya yake baadhi ya maeneo yanaoshikiliwa na waasi, baada ya idadi kubwa wanajeshi kujiodoa katika uwanja wa mapigano na kupelekea waasi kuendelea kuyadhibiti baadhi ya maeneo.

Mataifa ya magharibi na serikali ya Kiev, wamekua wakiinyooshea kidole Urusi, kuendelea kuwasaidia kijeshi waasi wanaoendelea kuyashikilia baadhi ya maeneo mashariki mwa Ukraine, tuhuma ambazo Urusi imekanusha.

Kwa mujibu wa mashahidi, jeshi la Ukraine limekua likijiondoa kwenye baadhi ya maeneo, na baadae maeneo hayo kudhibitiwa na waasi bila hata hivo kurushiana risase na waasi, hususan katika maeneo ya kusini mashariki ya jimbo la Donetsk , ambalo ni ngome ya waasi hadi kwenye mpaka wa Urusi, karibu na bandari muhimu ya Marioupol kusini mwa Ukraine.

Hata hivo, hivi karibuni waziri wa Ulinzi wa Ukraine amekua akionya dhidi ya vita ambavyo huenda vingelitokea kati ya Urusi na Ukraine, na “kusababisha vifo vya watu wengi”.

Tangazo hlo la kusitisha mapigano mashariki mwa Ukraine linatolewa mkesha wa mkutano wa jumuiya ya kujihami ya mataifa ya magharibi Nato, ambapo rais wa Ukraine anatazamiwa kukutana kwa mazungumzo na mwenziye wa Marekani Barack Obama, kabla ya kupokelewa Septemba 18 katiaka ikulu ya washington

Hayo yanajiri, wakati rais wa Marekani Barack Obama ameanza jumatano wiki hii ziara katika mji wa Tallinn kuhakikishia nchi za Baltic usalama wao baada ya mataifa hayo kuhofiwa kushambuliwa na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.