Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-Usalama

Ukraine: jeshi lazidiwa nguvu na waasi

Jeshi la Ukraine linaendela kupoteza baadhi ya maeneo na kuchukuliwa na waasi baada ya jeshi hilo kuanzisha hivi karibuni mashambulizi dhidi ya waasi kwa lengo la kuyaweka kwenye himaya yake maeneo yanayoshikiliwa.

Agosti 26 mwaka 2014, wanajeshi wa Ukraine walijiondoa katika uwanja wa ndege wa Lougansk, na baadae kutekwa na waasi.
Agosti 26 mwaka 2014, wanajeshi wa Ukraine walijiondoa katika uwanja wa ndege wa Lougansk, na baadae kutekwa na waasi. REUTERS/Gleb Garanich
Matangazo ya kibiashara

Waasi wameendelea kuyateka baadhi ya maeneo ukiwemo uwanja wa ndege wa Lougansk, ambao kwa sasa ni ngome yao. Tayari maafisa wa ngazi ya juu jeshini wameanza kunyooshewa kidole.

Kujiondoa kwa wanajeshi katika uwanja wa ndege wa Lougansk, ni moja ya ishara ya kushindwa kwa jeshi kumudu mapigano yanayoendeshwa na waasi. Kwa mujibu wa Volodymyr Rouban, ambaye ni afisa katika serikali ya Ukraine anaeshiriki mazungumzo ya kubadilishana wafungwa, takribani wanajeshi 700 wa Ukraine wameshikiliwa mateka hivi karibuni na waasi katika jimbo la Donetsk. Afisa huyo amebaini kwamba hali kwa sasa ni “tata”.

Wakati jeshi la Ukraine likijianda kuonesha sura nzuri ya kuimarisha ulinzi dhidi ya waasi, baadhi ya wanajeshi wamebaini kwamba wanakabiliwa na ukosefu wa uwezo, hususan vifaa vya jeshi. Bataliani moja ya wanajeshi imeamua kujiondoa katika uwanja wa mapigano hadi pale watapatishiwa uwezo wa kutosha wa kupambana vilivyo na waasi.

Wanajeshi wasio na uzowefu katika vita wametumwa katika uwanja wa mapigano, kama alivyoshuhudia mwanajeshi mmoja mwanamke.

Hata hivo, baadhi ya maseneta wa Marekani akiwemo rais wa halmashauri ya mambo ya nje kwenye bunge la Marekani, Robert Menendez, pamoja na baadhi ya wanasiasa wameomba jumatatu wiki hii kuitolea Ukraine msaada wa kijeshi ili iweze kupambana na waasi.

Uongozi wa jeshi wanyooshewa kidole cha lawama

Uongozi wa jeshi la Ukraine umeanza kutiliwa mashaka na namna jeshi limekua likishindwa kukabiliana na waasi katika uwanja wa mapigano. Baadhi ya wanajeshi wamekua wameelezea hasira zao dhidi ya uongozi wa jeshi na kuamua kutoendelea na mapigano hadi pale viongozi wa jeshi watajirekebisha kwa maamuzi wanayochukua.

Baadhi ya raia wa Ukraine wametoa maoni yao wakibaini kwamba uongozi wa jeshi ni dhaifu, wakiomba rais Petro Porochenko kuwafuta kazi viongozi wa jeshi kutokana na kutowajibika katika kazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.