Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-Mapigano-Usalama

Ukraine : Kiev yadai kushikilia magari ya kijeshi ya Urusi

Serikali ya Kiev imefahamisha alhamisi wiki hii kwamba imeshikilia vifaru viwili vya jeshi la Urusi, vilivyokamatwa na jeshi lake karibu na ngome ya waasi wa Ukraine katika mji wa Lougansk, ambapo jeshi la Ukraine linaendesha mapigano dhidi ya waasi.

Rais wa Ukraine,Petro Porochenko, akionesha jeshi lake silaha mpya walizopata kwa lengo la kuvunja uasi mashariki mwa Ukraine
Rais wa Ukraine,Petro Porochenko, akionesha jeshi lake silaha mpya walizopata kwa lengo la kuvunja uasi mashariki mwa Ukraine REUTERS/Mykhailo Markiv
Matangazo ya kibiashara

Iwapo taarifa hizo zitathibitishwa, itakua ni kwa mara ya kwanza kutolewa ushahidi kuhusu ushiriki wa jeshi la Urusi katika machafuko yanayoendelea kushuhudiwa mashariki mwa Ukraine.

Kiev imekua ikishtumu Urusi kuendeleza vita mashariki mwa Ukraine licha ya kua Moscow imeendelea kukanusha madai hayo. Ukraine, mara kadhaa imeinyoshea kidole Urusi kuhusu kushiriki kwake katika mapigano, hususan kuwapa waasi silaha na kuwasaidia waasio hao kijeshi.

“Katika mapigano ambayo yamekua yakiendelea karibu na mji wa Lougansk, jeshi la Ukraine limeteka vifaru vya jeshi la Urusi. Baadhi ya nyaraka, ikiwa ni pamoja na leseni ya uendeshaji gari na stakabadhi zingine za jeshi la Urusi vilikutwa ndani ya kifaru kimoja”, amesema msemaji wa jeshi la Ukraine, Andriï Lyssenko.

Waziri wa ulinzi wa Urusi, amekanusha madai hayo, akisema kwamba Ukraine imedai mara kadhaa kuwa ina ushahidi bila hata hivo kuonesha.
“Ni vigumu kuelewa iwapo kifaru cha jeshi kimekua ni maktaba, ambako kunakutwa stakabadhi zote hizo zisiyoeleweka, amesema msemaji wa jeshi la Urusi Igor Konachenkov.

Wakati huohuo jeshi la Ukraine linaendelea na mashambulizi dhidi ya mji wa Donetsk ili kujaribu kuwatimua waasi wanaoungwa mkono na Urusi, ambao wanaendelea kushikilia mji huo kwa mezi kadha sasa.

Mapigano hayo kati ya jeshi la Ukraine na waasi yanaripotiwa katika kijiji cha Makiïvka katika mji wa Donetsk. Mapigano hayo katika kijiji hicho yameingia kwa siku ya tatu alhamisi wiki hii, jeshi la ukraine likiwa na lengo la kuweka katika himaya yake kijiji cha Makiïvka kwa lengo la kukabiliana vilivyo na waasi waasi hao. Iwapo jeshi la Ukraine litafaulu kuteka kijiji cha Makiïvka, litakua limetamatisha operesheni yake ya kuuteka mji wa Donetsk.

Makiïvka ni eneo muhimu la waasi, ambalo linakabiliwa na mashambulizi ya jeshi la waasi. Lakini waasi wameapa kutoondoka katika kijiji hicho. Wakaazi wa Makiïvka, wamekimbia kijiji hicho wakihofiya usalama wao, huku baadhi ya raia wakikimbilia chini ya mashimo waliyochimba ndani ya nyumba zao.

Raia wengi wameuawa, huku idadi ya wakimbizi ikiendelea kuongezeka.Raia 40 wameuawa jumatano wiki hii katika mji wa Donetsk kufuatia mapigano yanayo endelea kati ya jeshi la Ukraine wakijaribu kudhibiti mji huo unaoshikiliwa kwa kipindi kirefu na waasi.

Hata hivo ndege ya kijeshi ya Ukraine imedunguliwa karibu na mji wa Lougansk, kwene umbali wa kilomita zaidi ya arobaini na mpaka wa Urusi. Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Ukraine, Andriï Lyssenko, haijafahamika ni akiana nani waliyodungua ndege, lakini amekiri kwamba ndege hiyo imedungulia na hatma ya rubani wa ndege hiyo haijafahamika.

Baadhi ya magari ya Urusi  yanayobeba msaada wa kibinadamu nchi Ukraine yakiruhusiwa kuvuka mpaka na kuingia nchini humo.
Baadhi ya magari ya Urusi yanayobeba msaada wa kibinadamu nchi Ukraine yakiruhusiwa kuvuka mpaka na kuingia nchini humo. REUTERS/Alexander Demianchuk

Hayo yakijiri baadhi ya magari ya Urusi yaliyokua yanabeba msaada wa kibinadamu nchini Ukraine, yameruhusiwa kuingia katika aridhi ya taifa hilo, baada ya kuzuiliwa mpakani kwa siku kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.