Pata taarifa kuu
UKRAINE-URUSI-MALAYSIA-Usalama wa anga

Ukaine : miili ya wahanga waliyokua ndani ya ndege ya Malaysia Airlines yasafirishwa

Miili 247 ya wahanga waliyofariki, baada ya ndege yenye chapa MH 17 ya Malaysia Airlines waliyokuwemo kudunguliwa katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi, imesafirishwa katika treni katika mji wa Torez unaoshikiliwa na waasi mashariki mwa Ukraine, msemaji wa wa wassi amethibitisha.

Mabaki ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines iliyopata ajali baada ya kudunguliwa karibu na eneo la Chakhtersk, katika jimbo la Donetsk,Julai 17 mwaka 2014.
Mabaki ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines iliyopata ajali baada ya kudunguliwa karibu na eneo la Chakhtersk, katika jimbo la Donetsk,Julai 17 mwaka 2014. REUTERS/Maxim Zmeyev
Matangazo ya kibiashara

“Wakati huu hakuna haja ya kutafuta treni ya pili”, waziri mkuu wa eneo lililojitenga la Donets, Alexandre Borodaï, ameambia shirika la habari la AFP, wakati ambapo serikali ya Kievi imesema kwamba treni ya pili yenye mabehewa 4 inaelekea katika mji wa Torez.

Naibu waziri mkuu wa eneo lililojitenga la Donets, Andreï Pourguine, ambaye amenukuliwa na shrika la habari la Urusi Interfax, amesema kwa upande wake kwamba miili ya wahanga itasafirishwa katika mji wa Kharkiv (eneo linaloshikiliwa na jeshi la serikali) endapo wataalamu wa kimataifa watakuwa wamewasili katika mji huo kuanzisha uchunguzi.

Kwa mujibu wa msemaji wa Borodaï, wataalamu kutoka Uholanzi wamewasili katika mji wa Donets, eneo muhimu kwa waasi. Hajafahamisha iwapo wataalamu hao watajielekeza katika eneo la tukio. Ndege hiyo ya Malaysia Airlines ilidunguliwa wakati ilipokua ikitokea Amsterdam ikiwa na abiriya 298, wengi wao wakiwa ni raia wa Uholanzi.

Eneo la tukio,  ilipopata ajali ndege ya Malaysia Airlines baada ya kudunguliwa katika jimbo la de Donetsk, Julai 17 mwaka 2014
Eneo la tukio, ilipopata ajali ndege ya Malaysia Airlines baada ya kudunguliwa katika jimbo la de Donetsk, Julai 17 mwaka 2014 REUTERS/Maxim Zmeyev

Timu ya wataalamu kutoka Uholanzi imewasili mapema jumatatu asubuhi wiki hii katika mji wa Kharkiv.

Hata hivo timu ya wataalamu kutoka Malatsia, imewasili mjini Kiev jana jumapili, na inasubiriwa katika mji wa Donets, ameendelea kusema msemaji wa Borodaï.

Katika tangazo liliyotolewa jumapili jioni, waziri wa usafiri wa Malaysia, Liow Tiong Lai, amekosoa vikali kauli ya viongozi wa Ukraine ya kukataa kuwalindia usalama wataalamu wa kimataifa katika eneo la tukio. Waziri huyo ameamuru usalama wa wataalamu wa kimataifa katika eneo la tukio uimarishwe vilivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.