Pata taarifa kuu
MYANMAR

Aung San Suu Kyi afanikiwa kunyakua ushindi katika uchaguzi wa ubunge

Kiongozi wa Upinzani nchini Myanmar ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Aung San Suu Kyi amefanikiwa kunyakua ushindi katika Uchaguzi wa Ubunge ambao umefanyika mwisho mwa juma hili.

REUTERS/Damir Sagolj
Matangazo ya kibiashara

Wanachama wa NLD Chama ambacho kinaongozwa na Aung San Suu Kyi walijikuta ni wenye furaha baada ya matokeo ya wali kuonesha kuwa Kiongozi wao ataingia Bungeni kwa mara ya kwanza kutetea maslahi yao.

Maelfu ya wanachama wa NLD wamesema huu ni wakati ambao ulikuwa unasubiri na wengi kwa Suu Kyi kuanza harakati za kutetea wananchi sambamba na kushinikiza mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo.

Wananchi wengi wanamatumaini Suu Kyi kuingia kwake kwenye Chombo cha Kutunga Sheria atasaidia pakubwa kuhakikisha wananchi wanapata haki zao ambazo zimekuwa zikikandamizwa na serikali ya kijeshi.

Kwa upande Suu Kyi mwenyewe amesema ushindi huo ni wa wananchi na si wa kwake yeye na ameahidi huu ni wakati muafaka wa kuanza kushinikiza utawala wa sheria katika nchi hiyo yenye misingi ya Utawala wa kijeshi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.