Pata taarifa kuu
Maldives

Mahakama nchini Maldives yatoa Waranti ya kukamatwa kwa Rais wa zamani wa Taifa hilo

Mahakama nchini Maldives imetoa waranti ya kukamatwa kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Nasheed ambaye anazuiliwa nyumbani kwake kwa sasa wakati huu ambapo machafuko yanazidi kushika kasi kupinga hatua kuondolewa kwake madarakani.

aliyekuwa Rais wa Visiwa vya Maldives, Mohamed Nasheed
aliyekuwa Rais wa Visiwa vya Maldives, Mohamed Nasheed ( Photo : AFP )
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa Nasheed wameendelea kupambana na askari ambao wanataka kurejesha utulivu katika nchi hiyo baada ya hali ya mambo kuchacha kufuatia Kiongozi huyo kulazimishwa kuondoka madarakani na jeshi.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mohamed Jameel Ahmed ameelekeza Shutuma kwa vyama vya siasa na viongozi kuwa ndiyo chanzo cha kutokea kwa machafuko yanayoshuhudiwa kwa sasa.

Kwa upande wake Nasheed ameona kitu muafaka kwa sasa kufanyika ni Vikosi vya Kulinda Amani kutoka Umoja wa Mataifa UN ndiyo vinaweza kuwa suluhu ya kushughulikia Mgogoro huo.

Tayari Umoja wa Mataifa UN umetuma ujumbe wake wakitaka machafuko hayo yashughulikiwe na hatimaye kurejesha utulivu uliopotea katika nchi hiyo kwa karibu juma moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.