Pata taarifa kuu
Yemeni

Milio ya risasi yasikika kwa siku ya pili nchini Yemeni

Milio ya risasi na mabomu vimeendelea kusikika nchini Yemen kwa siku ya pili mfululizo katika mji mkuu sanaa ambapo maelfu ya waandamanaji wameendelea kupambana na polisi.

Wanajeshi wa Yemeni na vifaa vya kijeshi tayari kupambana
Wanajeshi wa Yemeni na vifaa vya kijeshi tayari kupambana REUTERS / Khaled Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa licha ya kuwepo taarifa kuwa wanajeshi wa Serikali walikubaliana kusitisha mapigano dhidi ya wanajeshi waliojiunga na upinzani, bado mashambulizi dhidi ya raia yameendelea ambapo mpaka sasa watu 28 wamepoteza maisha.

Maaandamano hayo yanakuja ikiwa zimepita siku chache tangu rais Saleh amruhusu makamu wake wa rais kusaini makubaliano ya kupatikana serikali ya mpito nchini Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.