Pata taarifa kuu
PAKISTANI

Shambulizi la kujitoa mhanga nchini Pakistan laua watu zaidi ya 43

Shambulizi la Bomu la kujitoa mhanga lililotekelezwa kwenye Msikiti nchini Pakistani wakati wa sarat Ijumaa limesababisha vifo vya watu arobaini na tatu na kujeruhi wengine mia moja katika Wilaya ya Khyber.

IRNA
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo umetokea wakati msikiti huo unaopatikana katika Mji wa Jamrud ukiwa na waumini zaidi ya mia tano Mamlaka nchini Pakistani zimethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo.

Hofu imetanda huenda idadi ya vifo ikaongezeka kutokana na watu mia moja kumi na saba kujeruhiwa kwenye shambulizi hilo wengi wao vibaya na huu ni muendelezo wa matukio ya kujitoa mhanga ambayo yamekuwa yakitikisa nchi ya Pakistan.

Shambulizi hili ni la kwanza tangu waumini wa dini ya Kiislam nchini Pakistan wauangane na wenzao duniani kote katika kutekeleza ibada ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Afisa wa juu nchini Pakistan Khalid Mumtaz Kundi amenukuliwa akisema aliyejitoa mhanga alikuwa amebeba bomu lenye uzito wa kilo kati ya nane hadi kumi na kisha kukaa kwenye eneo la ibada.

Mashuhuda wa shambulizi hilo wamesema kuwa kijana mdogo ndiye alionekana akiwa amebeba bomu hilo muda mchache kabla ya kusikika kwa mlipuko huo kwenye msikiti wa Ijumaa.

Eneo ambalo limetokea shambulizi hilo linatajwa kama ngome imara kwa Wanamgambo wa Taliban na Mtando wa Al Qaeda uliojipa kulipiza kisasi kufuatia kuawa kwa Kiongozi wake Osama Bin Laden.

Mtandao wa Al Qaeda uliapa kuendelea kufanya mashambulizi zaidi kwenye nchi ya Pakistan baada ya Makomandoo wa Marekani kutekeleza shambulizi la kumua Osama ambaye inaelezwa alikuwa anaishi karibu na kambi ya mafunzo ya kijeshi.

Miezi mitatu sasa tangu kuanza upta kwa mashambulizi ya kujitoa mhanga kwenye nchi ya Pakistan ambayo imekuwa ikipita kipindi kigumu na kuchangia hata hali ya usalama kuwa tete zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.