Pata taarifa kuu
Yemen

Wanajeshi 100 wa Yemeni wapoteza maisha katika mapambano

Mapigano makali ambayo yameibuka kati ya majeshi ya serikali ya Yemeni dhidi ya Wanamgambo wanaodhaniwa ni wanachama wa Al Qaeda yamesababisha idadi ya vifo vya wanajeshi kufikia mia moja Kusini mwa Jiji la Zinjibar.

AFP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa zinaeleza wakati idadi ya vifo vya wanajeshi ikifika mia moja zaidi ya wengine mia mbili na sitini wamejeruhiwa wakati huu mapigano hayo yakiingia katika siku ya tatu tangu kuzuka upya.

Wanagambo hao ambao wenyewe wamejipa jina la Ansar Al Sharia wamekuwa wakitawala eneo la Zinjibar tangu mwezi May baada ya nchi hiyo kuingia kwenye shinikizo la kutaka Utawala wa Rais Ali Abdullah Saleh uondoke madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.