Pata taarifa kuu

Marekani: Republican washindwa kupitisha mswada wa bajeti ya muda mfupi

Nairobi – Shughuli za kawaida, zinaelekea kukwama nchini Marekani, baada ya chama cha Republican kushindwa kupitisha mswada wa bajeti ya muda mfupi. 

Ikulu ya White House imesema, hali hii inaweza kuzuiwa iwapo, wabunge wa Republican wataacha mgawanyiko ndani yao
Ikulu ya White House imesema, hali hii inaweza kuzuiwa iwapo, wabunge wa Republican wataacha mgawanyiko ndani yao AP - Ohad Zwigenberg
Matangazo ya kibiashara

Kushindikana kupitishwa kwa bajeti hiyo, kuna maanisha kuwa iwapo suluhu haitapatikana kwa saa chache zijazo, hakutakuwa na fedha za kuwalipa wafanyakazi kwenye mbunga za taifa za Wanyama, lakini pia itatiza ahadi ya Marekani kuisaidia Ukraine. 

Iwapo wabunge watashindwa kuafikia maelewano, hii itakuwa mara ya kwanza tangu mwaka 2019 kwa shughuli kukwama nchini Marekani, huku mamilioni ya wafanyakazi wakiwa kwenye hatari ya kutopata mishahara yao, wakiwemo maafisa wa kijeshi. 

Siku ya Ijumaa, wabunge wa Republican walishindwa kupitisha pendekezo la kiongozi wao Kevin McCarthy, ambaye pia ni Spika wa bunge, kitu kinachotazamwa kama ishara ya mgawanyiko ndani ya chama hicho kuelekea uchaguzi wa mwaka ujao. 

Ikulu ya White House imesema, hali hii inaweza kuzuiwa iwapo, wabunge wa Republican wataacha mgawanyiko ndani yao na kupitisha bejeti ya dharura. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.