Pata taarifa kuu

Brazili: Kimbunga chaua watu 41, 46 hawajulikani walipo

Mamlaka nchini Brazili imeongeza idadi ya watu waliotoweka kutoka 25 hadi 46 baada ya kimbunga kibaya kupiga kusini mwa nchi siku ya Jumatatu, ambacho kilisababisha vifo vya takribanwatu  41, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa siku ya Ijumaa usiku.

Uharibifu uliosababishwa na kimbuga kibaya katika la Rio Grande do Sul, Brazili.
Uharibifu uliosababishwa na kimbuga kibaya katika la Rio Grande do Sul, Brazili. AP - Wesley Santos
Matangazo ya kibiashara

Operesheni ya kujaribu kuwatafuta waliotoweka inaendelea, usalama wa raia wa jimbo la Rio Grande do Sul, kusini mwa majimbo 27 ya Brazil umesema katika taarifa.

Mvua kubwa na upepo mkali uliosababishwa na kimbunga hicho uliwalazimisha zaidi ya watu 11,000 kutoroka makazi yao. Zaidi ya watu 147,000 wameathiriwa, kulingana na makadirio ya hivi karibuni.

Majengo kadhaa yaliharibiwa na miji ikajaa maji kutokana na mafuriko. Jumla ya manispaa 87 ziliathiriwa, mamlaka imesema, ikiripoti majeruhi 223.

Gavana wa jimbo la Rio Grande do Sul, Eduardo Leite, siku ya Alhamisi alitembelea manispaa ya Muçum, ambayo ndiyo iliyoathiriwa zaidi na takriban watu 15 waliofariki na wengine 30 kupotea, na kuahidi kwamba intajengwa upya haraka iwezekanavyo.

"Tutahakikisha ujenzi mpya wa miji hii, miundombinu yake na maisha ya watu hawa", alithibitisha katika mkutano na waandishi wa habari Bw. Leite, akikadiria karibu dola milioni 20 za mahitaji ya kujenga upya miundombinu ya barabara.

Takriban waokoaji elfu moja na helikopta kadhaa zilitumwa kama sehemu ya shughuli za uokoaji, ambazo zilionekana kuwa ngumu siku ya Alhamisi baada ya madaraja mawili kuporomoka na kuziba kwa sehemu au jumla ya barabara kadhaa.

Mamlaka inatarajia hali mbaya ya hewa kuendelea kuwepo katika eneo hilo hadi Jumamosi asubuhi "kutokana na hali ya baridi kali" kutoka nchi jirani ya Uruguay.

Brazili mara nyingi hukumbwa na hali mbaya ya hewa, na wanasayansi wanaihusisha na athari za mabadiliko ya taianchi.

Mwezi Juni, kimbunga kiliua takriban watu 13 katika jimbo moja la Rio Grande do Sul.

Mnamo mwezi wa Februari, watu 65 waliangamia kufuatia maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyoikumba Sao Sebastiao, eneo la mapumziko la bahari yapata kilomita 200 kutoka Sao Paulo, kusini mashariki mwa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.