Pata taarifa kuu

Marekani: Florida yakumbwa na mvutano kufuatia sheria mpya kuhusu mafundisho ya utumwa

Idara ya Elimu katika jimbo la Florida nchini Marekani, inapitisha sheria mpya zinazopingwa vikali kuhusu kufundisha utumwa katika shule za umma. Sheria hizi mpya zinawataka walimu hasa kuwafundisha wanafunzi wao kwamba utumwa uliwaruhusu watumwa "kukuza ujuzi". Upinzani kutoka chama cha Democratic unalaani hatua hii na kusema ni kurejelea mambo yaliyopitwa na wakati.

Kamishna wa Elimu katika jimbo la Florida Manny Diaz.
Kamishna wa Elimu katika jimbo la Florida Manny Diaz. © wikimédia
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Miami, David Thomson

Hati hii ya kurasa 200 inaeleza kwa kina miongozo mipya ya mtaala ya kufundisha historia ya utumwa, ubaguzi wa rangi na Wamarekani wenye asili ya Afrika katika shule za Florida.

Hati hiyo kwanza inapendekeza kuangazia ushawishi chanya wa Wamarekani wenye sifa kama vile Martin Luther King, Rosa Parks au Barack Obama... Lakini pale ambapo Idara ya Elimu ya Florida inazusha utata, ni pamoja na maagizo yake inayopendekeza walimu kuwafundisha wanafunzi kwamba watumwa walikuwa na "ujuzi mkubwa" ambao waliweza "kutumia kwa manufaa yao binafsi".

Kifungu kingine kinachopingwa sana: ni kile kuhusu mafundisho ya uhalifu wa rangi ambayo, kulingana na sheria mpya za elimu za Florida, "ulifanywa dhidi ya watu weusi lakini pia na Wamarekani-wenye asili ya Afrika".

'Hatua kubwa kurudi nyuma'

Sheria hizi mpya zilipigiwa kura siku ya Alhamisi na Idara ya Elimu inayoongozwa na Manny Diaz, rafiki wa karibu wa Gavana Ron DeSantis, mpinzani mkuu wa Donald Trump katika kura za mchujo za chama cha Republican ambaye ameahidi kukomesha kile anachokiita "endoctrinement woke" katika elimu ya umma.

Kwa upande wake, upinzani umeghadhabishwa na hatua hii. "Nimeshangaa kwamba Florida bado inahalalisha utumwa mnamo mwaka 2023," afisa mteule Shevrin Jones, mwenyewe mweusi na mwalimu amesema. Chama kikuu cha walimu kinakashifu kile ambacho imeita, "Marekani inapiga hatua kubwa kurudi nyuma".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.