Pata taarifa kuu

Marekani: Mahakama ya juu yafuta sera ya vyuo vikuu kuwasajili wanafunzi kwa upendeleo

Nairobi – Mahakama ya Juu ya nchini Marekani, imeagiza kuondolewa  kwa sera ya muda, ambayo imekuwa ikitoa fursa kwa watu kutoka makundi yaliyotengwa, kujiunga na vyuo vikuu nchini humo kwa kuzingatia rangi yao, kwa kile inachosema inakiuka katiba. 

Mahakama ya juu nchini Marekani siku ya Alhamisi ilipiga marufuku ubaguzi wa rangi na kabila wakati wa kujiunga na vyuo vikuu. (Picha na OLIVIER DOULIERY / AFP)
Mahakama ya juu nchini Marekani siku ya Alhamisi ilipiga marufuku ubaguzi wa rangi na kabila wakati wa kujiunga na vyuo vikuu. (Picha na OLIVIER DOULIERY / AFP) AFP - OLIVIER DOULIERY
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umetolewa na Majaji sita kati ya watatu, wa Mahakama hiyo. Waliounga kufutwa kwa sera hiyo ni Majaji walioteuliwa na rais wa zamani Donald Trump. 

Tangu miaka ya sitini, sera ya kutoa fursa kwa watu wakiwemo weusi, kujiunga na vyuo kama Harvard na North Carolina, ili kupata fursa ya kupata elimu imekuwa ikitumika. 

Majaji waliounga mkono uamuzi huo, wakiongozwa na Jaji Mkuu John Roberts, wamesema kwa muda mrefu vyuo vikuu vimekuwa vikitumia sera hiyo kimakosa, na kuzitaka taasisi hizo za elimu ya juu kutafuta njia mbadala ya kuwaandikisha wanafunzi bila kuzingatia rangi na asili ya kule wanakotokea. 

Uamuzi huu umepokelewa kwa  kwa hisia mseto na Wamarekani  huku rais Joe Biden akiulaani na kusema ni ishara kuwa ubaguzi bado upo Marekani na kuongeza kuwa vyuo vikuu nchini humo vinakuwa imara vikiwa na wanafunzi kutoka matabaka mbalimbali. 

Maandamano pia yameshuhudiwa mbele ya Mahakama hiyo baada ya uamuzi kuonesha hasira zao, wakisema  maamuzi hayo hayakubaliki. 

Hata hivyo, rais wa zamani Trump ambaye ametangaza nia ya kuwania urais mwaka ujao, amewasifu Maji wa Mahakama ya juu na kusema uamuzi wao, unatoa haki kwa usawa kwa Wamarekani. 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.