Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Donald Trump akana mashtaka katika mahakama ya shirikisho

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, anayeshtakiwa kwa uzembe wake wa kushughulikia siri za serikali baada ya kuondoka Ikulu ya White House, amekana mashtaka dhidi yake siku ya Jumanne, Juni 13 wakati wa kufikishwa kwake katika mahakama ya shirikisho huko Miami.

Msafara wa Donald Trump katika mahakama ya shirikisho huko Miami mnamo Juni 13.
Msafara wa Donald Trump katika mahakama ya shirikisho huko Miami mnamo Juni 13. Getty Images via AFP - ALON SKUY
Matangazo ya kibiashara

"Bila shaka hatuna hatia," alisema Todd Blanche, wakili wa Donald Trump wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo. Hii inafungua njia kwa ajili ya kesi inayoweza kuharibu sana kampeni yake kwa uchaguzi wa urais wa Marekani wa :mwaka 2024. Naye Donald Trump alishutumu "matumizi mabaya ya mamlaka" mbele ya wafuasi wake waliokusanyika kwenye klabu yake ya gofu huko New Jersey. Kisha alimshutumu mrithi wake wa chama cha Democratic Joe Biden kwa kuwa "mfisadi" na kumshambulia "mpinzani wake mkuu wa kisiasa". "Ni kuingilia uchaguzi," aliongeza.

Rais huyo wa zamani wa chama cha Republican mwenye umri wa miaka 76 anatuhumiwa kuhatarisha usalama wa Marekani kwa kutunza nyaraka za siri, ikiwa ni pamoja na mipango ya kijeshi au taarifa kuhusu silaha za nyuklia, katika bafu au chumba cha kuhifadhia nyaraka zake binafsi katika makazi yake ya kifahari ya Mar-a-Lago, Florida.

Pia anashutumiwa kwa kukataa kurudisha hati hizi licha ya agizo ya mahakama, ambazo zilimfanya ashtakiwe kwa "kuhifadhi kinyume cha sheria taarifa zinazohusiana na usalama wa taifa", lakini pia "kuzuia mahakama kufanya kazi yake" na "ushahidi wa uongo". Jaji wa shirikisho alimjulisha siku ya Jumatano kuhusu mashtaka 37 dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.