Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Shambulizi la silaha nchini Ecuador laua watano na wanane kujeruhiwa

Takriban watu watano waliuawa na wanane kujeruhiwa Jumapili wakati wanaume watatu walipofyatua risasi ndani ya nyumba huko Guayaquil, mojawapo ya miji iliyoathiriwa zaidi na uhalifu na ulanguzi wa dawa za kulevya nchini Ecuador, polisi imesema usiku wa kuamkia leo Jumatatu.

Mwanajeshi wa Ecuador huko Esmeraldas, Aprili 21, 2023.
Mwanajeshi wa Ecuador huko Esmeraldas, Aprili 21, 2023. © ENRIQUE ORTIZ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashahidi, wanaume watatu waliokuwa kwenye pikipiki walifika katika eneo la Isla Trinitaria, kusini mwa jiji hilo, na kuingia ndani ya nyumba hiyo ambapo "walifyatua risasi kadhaa". "Hadi sasa, tumehesabu watu watano waliofariki na wanane kujeruhiwa," afisa mwenye cheo cha kanali katika polisi Fabary Montalvo amewaambia waandishi wa habari. 

Mmoja wa waliofariki ni afisa wa polisi aliyepigwa risasi mara kadhaa kichwani, amesema. Ecuador, mzalishaji mkubwa zaidi wa kokeini duniani, ambayo inapatikana kati ya Colombia na Peru,  inakumbwa na ongezeko mbaya zaidi la vurugu katika historia yake ya hivi majuzi. Uhalifu unaohusiana na dawa za kulevya umesababisha kiwango cha mauaji kuongezeka karibu mara mbili kati ya mwaka 2021 na 2022, kutoka 14 hadi 25 kwa kila watu 100,000. 

Mnamo Mei 25, takriban watu sita walikufa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kufyatua risasi kwenye mgahawa katika mji wa kitalii wa Montañita. Siku mbili kabla, watu wenye silaha waliingia katika chumba cha kuhifadhia maiti katika bandari iliyo karibu ya Manta na kuwafyatulia risasi waliohudhuria hafla ya mazishi, na kuua wanne na kujeruhi wanane. 

Mamlaka zinahusisha ghasia hizo na migogoro kati ya magenge na makundi ya walanguzi wa madawa ya kulevya kuhusu udhibiti wa njia za usafirishaji haramu wa binadamu katika Bahari ya Pasifiki, njia ya kimkakati ya usafirishaji wa dawa za kulevya Marekani na Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.