Pata taarifa kuu
ECUADOR-USALAMA

Ecuador: Makabiliano kati ya makundi hasimu yaua zaidi ya watu 100 jela

Rais wa Ecuador Guillermo Lasso Jumatano usiku ametangaza "hali ya hatari" katika magereza yote ya Ecuador, siku moja baada ya mapigano kati ya magenge hasimu ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 100 katika jela moja kusini magharibi mwa nchi hiyo Septemba 28.

Askari wakitoa ulinzi mbele ya mlango wa jela la Guyaquil ambapo mapigano kati ya wafungwa yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 100 Septemba 28, 2021.
Askari wakitoa ulinzi mbele ya mlango wa jela la Guyaquil ambapo mapigano kati ya wafungwa yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 100 Septemba 28, 2021. AP - Angel DeJesus
Matangazo ya kibiashara

"Nimetangaza hali ya hatari atika magereza yote nchini", aamesema Guillermo Lasso kwenye ukurasa wake wa Twitter, wakati magereza ya Ecuador kwa miezi kadhaa yamekuwa yakikumbwa vurugu za mara kwa mara kati ya makundi ya wahalifu yanayohusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya. "Huko Gayaquil, nitasimamia kamati ya usalama inayohusika na kuratibu hatua zinazohitajika kudhibiti dharura, kwa kuhakikisha haki za binadamu za kwa watu wote waliohusika zinaheshimishwa," ameongeza.

Makabiliano haya ya hivi karibuni, ambayo ni mabaya zaidi mwaka huu, yalifanyika katika jela kuu la Guayas, huko Guayaquil, mji wa bandari na kitovu cha biashara kusini magharibi mwa nchi. "Zaidi ya wafungwa 100 waliuawa na 52 walijeruhiwa" wakati wa vurugu, mamlaka ya magereza (SNAI) ilitangaza Jumatano jioni.

Ripoti ya awali, iliyotolewa na kamanda wa polisi wa Guayaquil, Jenerali Fausto Buenano, ambaye aliongoza operesheni hizo kudhibiti tena majengo ya jela, ilibaini kwamba wafungwa 30 waliouawa katika mapigano haya, sita kati yao walikatwa vichwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.