Pata taarifa kuu

Marekani yakanusha kuhusika na madai ya jaribio la kumuua Putin

NAIROBI – Ikulu ya Marekani, imekanusha madai yaliyotolewa na Serikali ya Moscow kuwa, nchi yake inahusika pakubwa katika kupanga shambulio la ndege isiyo na rubani, ambayo ilidunguliwa juma hili na vikosi vya Urusi.

Msemaji wa baraza la usalama wa taifa nchini Marekani, John Kirby
Msemaji wa baraza la usalama wa taifa nchini Marekani, John Kirby REUTERS - EVELYN HOCKSTEIN
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa baraza la usalama wa taifa nchini Marekani, John Kirby, amesisitiza nchi yake kutohusika akisema hata wapo wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo.

“ Urusi imekuwa ikijaribu kuchora picha ya mzozo unaoendelea kama vita kati ya nchi za magharibi dhidi ya Urusi, NATO dhidi ya Urusi, Marekani dhidi ya Urusi, kwa hivyo hii ni dhahiri ya mpango wake.” Amesema John Kirby, Msemaji wa baraza la usalama wa taifa nchini Marekani.

00:34

John Kirby, Kuhusu mzozo wa Urusi na Ukraine

Juma hili pia utawala wa Kiev umekanusha tuhuma za Urusi kuwa ilijaribu kumuua rais Vladmir Putin.

Ukraine juma hili imeendelea kusisitiza kuwa ni lazima mahakama maalumu iundwe kuwawajibisha na kuchunguza uhalifu uliotekelezwa na Urusi kwenye ardhi yake.

Ukraine inataka rais Vladimir Putin kufikishwa katika mahakama ya The Hague
Ukraine inataka rais Vladimir Putin kufikishwa katika mahakama ya The Hague AP - Mikhail Klimentyev

Akiwa mjini the Hague, Uholanzi, rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amesema ni muhimu kwa chombo hicho kuundwa ili kuiwajibisha Moscow kutokana na uhalifu inaoendelea kutekeleza.

“Bila shaka tunataka kumuona Putin hapa Hague, anapashwa kufungwa hapa kwenye mji wa sheria za kimataifa.” Alisema rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

00:20

Rais Zelensky wa Ukraine kuhusu Putin kufikishwa Hague

Zelensky alisema haya wakati alipofanya ziara ya kushtukiza mjini The Hague, Uholanzi.

Volodymyr Zelensky wiki hii amezuru mahakama ya kimataifa ya uhalifu The Hague nchini Uholanzi
Volodymyr Zelensky wiki hii amezuru mahakama ya kimataifa ya uhalifu The Hague nchini Uholanzi AFP - PHIL NIJHUIS

Mahakama hiyo ilikuwa imetoa kibali cha kukamatwa kwa rais Putin akihusishwa na vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu nchini Ukraine baada ya wanajeshi wake kuivamia nchi hiyo.

Utawala wa Kremlin umekuwa ukizituhumu nchi za magharibi na washirika wa Ukraine kwa kuingilia mzozokati kati ya Kyiv na Moscow, rais Putin akizionya nchi hizo kwa kuendelea kuihami Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.